Rais Sisi wa Misri aidhinisha sheria ya kuwazuia wanajeshi kuwania urais
(last modified Thu, 30 Jul 2020 10:33:45 GMT )
Jul 30, 2020 10:33 UTC
  • Rais Sisi wa Misri aidhinisha sheria ya kuwazuia wanajeshi kuwania urais

Rais Abdul Fattah al-Sisi wa Misri ameidhinisha sheria ya kupiga marufuku wanajeshi walio kazini na waliostaafu kuwania urais au ubunge bila idhini ya jeshi.

Sheria hiyo mpya inakuja baada  ya Wamisri kupiga kura mwaka jana kuidhinisha mabadiliko ya katiba ambayo yatamuwezesha al-Sisi, ambaye ni jenerali wa zamani jeshini, kubakia madarakani hadi mwka 2030.

Sheria mpya iliyopitishwa Jumatano itafanya iwe viumu sana kwa maafisha wa kijeshi kugombea kiti chochote cha kisiasa na kwa msingi huo kuwazuia wapinzani wenye nguvu kuibuka dhidi ya al-Sisi.

Tokea Misri iwe jamhuri ya kisasa, marais wake wote isipokuwa wawili walikuwa ni wanajeshi.

Al-Sisi zama zake jeshini

Al-Sisi aliongoza mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa Muhammad Morsi madarakani mwaka 2013. Morsi, ambaye alifariki dunia akiwa gerezani, alikuwa rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia Misri.

Mkuu wa zamani wa majeshi ya Misri, Sami Anan, alifungwa jela Januari 2018 baada ya kujitokeza kugombea urais dhidi ya al-Sisis bila idhini ya jeshi. Aliachiliwa huru miaka miwili baadaye.

 

Tags