Watu wawili wauawa Ivory Coast baada Ouatarra kutangaza kugombea tena urais
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i62998-watu_wawili_wauawa_ivory_coast_baada_ouatarra_kutangaza_kugombea_tena_urais
Watu wawili wameuwawa katika machafuko ya kikabila nchini Ivory Coast baada ya rais Alassane Ouattara kutangaza kwamba atawania muhula wa tatu madarakani.
(last modified 2025-11-18T07:21:20+00:00 )
Aug 24, 2020 07:15 UTC
  • Watu wawili wauawa Ivory Coast baada Ouatarra kutangaza kugombea tena urais

Watu wawili wameuwawa katika machafuko ya kikabila nchini Ivory Coast baada ya rais Alassane Ouattara kutangaza kwamba atawania muhula wa tatu madarakani.

Wafuasi vijana wa upinzani waliandamana hapo jana katika miji kadhaa nchini humo hasa katika mji unaozalisha kwa wingi zao la kakao wa Divo kupinga uamuzi wa Ouattara baada ya kuafiki kugombea urais katika uchaguzi wa Oktoba.

Ouattara aliteuliwa rasmi Jumamosi kama mgombea kupitia chama chake cha RHDP licha ya kuhudumu mihula miwili madarakani ambayo ndio inayokubalika chini ya katiba ya nchi hiyo.

Ouatarra alikuwa amepanga kumkabidhi hatamu za uongozi waziri mkuu Amadou Gon Coulibaly ambaye alifariki kwa mshtuko wa moyo mwezi Julai.

Tayari watu sita walikuwa wamefariki katika maandamano baada ya Ouattara kutangaza Agosti sita kuwa kuna uwezekano akagombea tena urais.

Rais Alassane Ouattara wa Ivory Coast

Wapinzani Ivory Coast wanapinga hatua ya Ouattara kugombea kiti cha rais kwa mara ya tatu. Hata hivyo Alassane Ouattara mwenyewe na chama tawala cha RHDP wanaamini kuwa, "Jamhuri ya Tatu" imeanza nchini humo na kwamba yeye ni mgombea wa kwanza katika jamhuri hiyo ya Ivory Coast baada ya kufanyiwa marekebsho katiba ya nchi mwaka 2016.