Watu wawili wengine wauawa nchini Burundi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i7795-watu_wawili_wengine_wauawa_nchini_burundi
Watu wasiojulikana wenye silaha wameshambulia ofisi ya chama tawala cha CNDD-FDD katika wilaya ya Ndava huko Mwaro nchini Burundi na kuuawa polisi mmoja na raia mwengine mmoja.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 25, 2016 08:55 UTC
  • Watu wawili wengine wauawa nchini Burundi

Watu wasiojulikana wenye silaha wameshambulia ofisi ya chama tawala cha CNDD-FDD katika wilaya ya Ndava huko Mwaro nchini Burundi na kuuawa polisi mmoja na raia mwengine mmoja.

Shirika la habari la France Press limeripoti habari hiyo na kumnukuu mkuu wa Wilaya ya Ndava, Jean-Marie Nyakarerwa akithibitisha habari hiyo na kuongeza leo kuwa, watu wenye silaha, usiku wa kuamkia leo Jumatano wameivamia ofisi ya chama tawala katika wilaya ya Ndava uvamizi ambao umepelekea kwa uchache polisi mmoja na raia mmoja kuuawa na watu wengine wanne kujeruhiwa.

Nchi hiyo ndogo ya katikati mwa Afrika imekumbwa na machafuko kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Machafuko hayo yalianza mwezi Aprili mwaka jana, wakati chama tawala cha CNDD-FDD kilipomteua Rais Pierre Nkurunziza kugombea uraia kwa mara ya tatu mfululizo.

Mashambulizi na mauaji ya kulipiza kisasi yamekuwa yakitokea mara kwa mara katika maeneo tofauti ya Burundi.