Waislamu wa Nigeria waadhimisha kumbukumbu ya mauaji ya Zaria
(last modified Mon, 13 Dec 2021 08:19:47 GMT )
Dec 13, 2021 08:19 UTC
  • Waislamu wa Nigeria waadhimisha kumbukumbu ya mauaji ya Zaria

Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Nigeria wameadhimisha kumbukumbu ya mwaka wa sita tangu yalipotokea mauaji ya kinyama yaliyofanywa na vyombo vya usalama vya Nigeria dhidi ya Waislamu katika mji wa Zaria

Maadhimisho hayo yamefanyika katika mji mkuu wa Nigeria Abuja na kuhutubiwa na Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria pamoja na wajumbe waandamizi wa harakati hiyo.

Akihutubia katika kumbukumbu hiyo, Sheikh Ibrahim Zakzaky ameashiria mauaji ya Waislamu wa Nigeria katika mji wa Zaria na kusema: Jamii yetu ya sasa ambayo maisha yao yameharibika, kwa nini watu walioko madarakani wanadhani kwamba, wana haki ya kuwaua watu wakati wowote watakao.

Sheikh Zakzaky ameashiria udharura wa watu kuishi pamoja na na kubainisha kwamba, sduala la kweko sheria na kuheshimiwa ni jambo la lazima pia. 

Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria

 

Katika shambulio hilo la Disemba 12, 2015, inakadiriwa wanachama zaidi ya 1,000 wa harakati ya Kiislamu ya Nigeria, aghalabu wakiwa ni Waislamu wa madhehebu ya Shia waliuawa kwa kufyatuliwa risasi na jeshi la Nigeria. Miongoni mwa waliouawa walikuwemo watoto watatu wa kiume wa Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria.

Katika siku iliyofuata, Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe Malama Zeenat walitiwa nguvuni wakati wanajeshi wa Nigeria walipovamia Hussainia ya Baqiyatullah na nyumba ya mwanazuoni huyo katika mji wa Zaria.

Hatua kandamizi na za kikatili za polisi na jeshi la Nigeria dhidi ya wafuasi wa Sheikh Zakzaky zingali zinaendelea na hadi sasa idadi kubwa ya wafuasi wa kiongozi huyo wa kidini wamewekwa kizuizini au wameuawa shahidi.