Masharti ya Waziri Mkuu wa Libya kwa ajili ya kukabidhi madaraka
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i80154-masharti_ya_waziri_mkuu_wa_libya_kwa_ajili_ya_kukabidhi_madaraka
Waziri Mkuu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya amesisitiza kuwa baraza lake la mawaziri litaendelea kufanya kazi hadi wakati wa kukabidhiwa madaraka kwa serikali iliyochaguliwa na wananchi.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Feb 09, 2022 08:03 UTC
  • Masharti ya Waziri Mkuu wa Libya kwa ajili ya kukabidhi madaraka

Waziri Mkuu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya amesisitiza kuwa baraza lake la mawaziri litaendelea kufanya kazi hadi wakati wa kukabidhiwa madaraka kwa serikali iliyochaguliwa na wananchi.

Kwa mujibu wa ripoti ya leo Jumatano ya shirika la habari la ISNA, Waziri Mkuu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya, Abdul Hamid Al-Dubeiba, katika hotuba yake kwa watu wa nchi hiyo, amongeza kuwa atakabidhi tu madaraka kwa serikali itakayochaguliwa wananchi wa nchi hiyo katika uchaguzi ujao.

Al-Dabiba amesema: "Watu wana utukufu na heshima yao, na wamechoshwa na uwepo wa miaka mingi wa wabunge kwenye viti vya bunge. Tunaunga mkono uchaguzi na tunapinga kurefushwa kwa bunge."

"Kamwe hatutaruhusu tabaka tawala la kisiasa kuendelea kutawala katika miaka ijayo," amesema waziri mkuu huyo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya.

Uchaguzi Libya

Matamshi ya Al-Dabeiba yametolewa katika kujibu hatua ya bunge la Libya siku ya Jumatatu ya kuidhinisha mapendekezo ya kamati ya bunge kwa ajili ya awamu ijayo ya nchi hiyo.

Spika wa Bunge la Libya Aqila Saleh hivi karibuni alitoa wito wa kuundwa serikali mpya, akitangaza kuwa serikali ya al-Dubai imekuwa haina mamlaka ya kisheria tangu Desemba 24, kufuatia uamuzi wa bunge wa kutokuwa na imani nayo.