Buhari: Jeshi la Nigeria litaendelea kupambana na wanamgambo wa Niger Delta
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i8086-buhari_jeshi_la_nigeria_litaendelea_kupambana_na_wanamgambo_wa_niger_delta
Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria amesema kuwa, serikali ya nchi hiyo itaendelea kusisitiza umuhimu wa kuendelezwa mapambano dhidi ya waasi wa eneo la Niger Delta nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 30, 2016 00:09 UTC
  • Buhari: Jeshi la Nigeria litaendelea kupambana na wanamgambo wa Niger Delta

Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria amesema kuwa, serikali ya nchi hiyo itaendelea kusisitiza umuhimu wa kuendelezwa mapambano dhidi ya waasi wa eneo la Niger Delta nchini humo.

Buhari aliyasema hayo jana Jumapili kupitia hotuba yake ya mwaka na kuongeza kuwa, serikali yake itaendeleza mapambano dhidi ya washambuliaji wa taasisi za mafuta za nchi hiyo. Rais Buhari pia ameahidi kulinda taasisi hizo za mafuta huku akitaka kufanya mazungumzo na viongozi wa eneo hilo kwa lengo la kutatua mgogoro huo ambao hadi sasa umeisababishia serikali ya Abuja, hasara ya mamilioni ya Dola. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, askari wa baharini katika eneo hilo wamepewa jukumu la kushirikiana na askari wa kikosi maalumu, kukabiliana na wanamgambo wa kundi la Ulipizaji Kisasi wa Niger Delta ambao kwa muda sasa wamekuwa wakishambulia taasisi za mafuta katika eneo hilo.