Jun 05, 2016 03:47 UTC
  • Jitihada za serikali ya Kongo Brazaville katika kupambana na ufisadi

Serikali ya Jamhuri ya Kongo au Kongo Brazaville imesema kuwa ufisadi wa fedha unaoikabili nchi hiyo unakwamisha ustawi wa kiuchumi na kijamii nchini humo.

Serikali ya Jamhuri ya Kongo imesema kuwa wanajiandaa kufanya marekebisho ili kuweza kupambana na ufisadi, rushwa na ubadhirifu. Hii ni kwa sababu masuala kama hayo yanadumaza ustawi wa kiuchumi na hata kijamii. Clemente Mouamba Waziri Mkuu wa Kongo Brazaville amesema kuwa tayari amewasilisha bungeni mpango wa marekebisho wa kupambana na ufisadi ili uchunguzwe na kisha kuidhinishwa. Clemente Mouamba ameeleza kuwa, licha ya kuwepo taasisi za kupambana na ufisadi wa fedha na kamisheni ya taifa ya kupambana na rushwa na ubadhirifu, lakini kutoheshimiwa misingi ya kiakhlaqi katika jamii, kumeifanya serikali ilazimike kuwasilisha mabadiliko hayo kwa sababu ufisadi wa fedha umekuwa saratani kwa jamii.

Polisi, mawakala wa forodha, wafanyakazi wa idara za kodi, manispaa ya miji na hospitali wanahusika pakubwa katika vitendo vya rushwa na ufisadi wa fedha nchini Kongo Brazaville.

Tags