Amir-Abdollahian asisitiza utekelezwaji mapatano ya Iran na Tanzania
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i87474-amir_abdollahian_asisitiza_utekelezwaji_mapatano_ya_iran_na_tanzania
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuhusu utekelezwaji wa mapatano yaliyofikiwa katika kikao cha kwanza cha Tume ya Pamoja ya Ushirikiano wa Iran na Tanzanjia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 27, 2022 03:03 UTC
  • Amir-Abdollahian asisitiza utekelezwaji mapatano ya Iran na Tanzania

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuhusu utekelezwaji wa mapatano yaliyofikiwa katika kikao cha kwanza cha Tume ya Pamoja ya Ushirikiano wa Iran na Tanzanjia.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Hossein Amir-Abdollahian aliyasema hayo Ijumaa mjini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Liberata Mulamula.

Katika kikao hicho Amir-Abdollahian alisema moja ya masuala yanayohitajika katika ustawi wa uhusiano ni kutatuliwa kadhia ya visa kwa wafanyabiashara wa Iran nchini Tanzania.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran pia alibainisha kuhusu mazungumzo ya kuondolewa Iran vikwazo na kusema:"Iwapo Marekani itazingatia uhalisia wa mambo basi kuna uwezekano wa kutekelezwa mapatano yaliyopita kwa masharti mapya."

 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aliwasili Tanzania Jumatano akitokea Mali katika safari yake barani Afrika. Akiwa mjini Dar es Salaam,  Alhamisi alishiriki katika kikao cha biashara baina ya Iran na Tanzania. 

Ijumaa pia Waziri wa Mambo ya Nje wa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alikutana na kufanya mazungumzo na Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma na pia akiwa mjini Zanzibar siku hiyo hiyo alikutana an kufanya mazungumzo na Rais Hussein Mwinyi wa Zanzibar.