Algeria yazialika harakati za Hamas na Fat'h kushiriki mazungumzo na maelewano
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i88320-algeria_yazialika_harakati_za_hamas_na_fat'h_kushiriki_mazungumzo_na_maelewano
Algeria imetangaza kuwa, imewaalika viongozi Wapalestina wa harakati za Hamas na Fat'h kushiriki katika mazungumzo ya maelewano ya kitaifa mjini Algiers.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 18, 2022 22:08 UTC
  • Algeria yazialika harakati za Hamas na Fat'h kushiriki mazungumzo na maelewano

Algeria imetangaza kuwa, imewaalika viongozi Wapalestina wa harakati za Hamas na Fat'h kushiriki katika mazungumzo ya maelewano ya kitaifa mjini Algiers.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kuhusu suala hilo, harakati za Hamas na Fat'h zimepokea barua rasmi za mwaliko kushiriki katika mazungumzo ya maelewano ya kitaifa ya Palestina.

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetoa shukrani zake za dhati kwa Algeria kutokana na azma ya wakuu wa Algeria ya kuhimiza mazungumzo ya maelewano ya kitaifa ya Palestina.

Harakati ya Fat'h nayo pia imesisitiza kuwa itatoa jibu chanya kwa mwaliko wa Algeria na kuongezwa kuwa umoja ndio njia pekee ya kulinda malengo ya ukombozi wa Palestina.

Huko nyuma pia Algeria iliwahi kuandaa mikutano ya  maeleno ya kitaifa baina ya makundi ya Palestina  ambapo mkutano huyo ulileta pamoja Hamas, Fat'h, Jihad Islami, Harakati ya Wananchi kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina, Harakati ya Wananchi-Kamandi Kuu.

Makundi ya kitaifa na Kiislamu Palestina yametangaza kuwa, maelewano ya kitaifa ni chaguo bora zaidi la kurejesha itibari ya taifa la Palestina na ni stratijia ya kitaifa ambayo makundi ya Kipalestina yanaafiki.