Vikosi vya ulinzi vya Nigeria vyalaumiwa kwa kukandamiza raia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i8878-vikosi_vya_ulinzi_vya_nigeria_vyalaumiwa_kwa_kukandamiza_raia
Shirika la kimataifa la haki za binadamu la Amnesty International limevilaumu vyombo vya ulinzi vya Nigeria kwa kukandamiza waandamanaji wasio na silaha.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 10, 2016 02:53 UTC
  • Vikosi vya ulinzi vya Nigeria vyalaumiwa kwa kukandamiza raia

Shirika la kimataifa la haki za binadamu la Amnesty International limevilaumu vyombo vya ulinzi vya Nigeria kwa kukandamiza waandamanaji wasio na silaha.

Shirika la habari la Ufaransa limeinukuu Amnesty International ikisema leo kuwa, vikosi vya ulinzi vya Nigeria vimewakandamiza wanaharakati wa harakati moja ya kupigania uhuru isiyo na silaha ambayo ilipanga kufanya maandamano ya kukumbuka mapigano ya ndani ya Biafra.

Shirika la Amnesty International limenukuu taarifa za jeshi la polisi la Nigeria na kusema kuwa, katika machafuko ya tarehe 30 Mei ya maandamano ya kukumbuka kuanza vita vya ndani vya Biafra huko Nigeria, watu 10 waliuawa ambapo watano waliuawa katika mji wa Onitsha wa jimbo la Anambra la kusini mwa Nigeria na watano wengine walikufa katika mji wa Asaba wa jimbo la Delta la kusini mashariki mwa nchi hiyo.

Harakati ya wananchi wa Biafra imekuwa ikifanya maandamano ya mara kwa mara huko kusini mashariki mwa Nigeria tangu alipotiwa mbaroni mkuu wa harakati hiyo Nnamdi Kanu mwezi Oktoba mwaka jana kwa tuhuma za usaliti.