AU kutuma waangalizi wa uchaguzi nchini Uganda
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i895-au_kutuma_waangalizi_wa_uchaguzi_nchini_uganda
Umoja wa Afrika umetangaza kuwa utatuma waangalizi wa uchaguzi kufuatilia zoezi la upigaji kura nchini Uganda.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 09, 2016 04:54 UTC
  • AU kutuma waangalizi wa uchaguzi nchini Uganda

Umoja wa Afrika umetangaza kuwa utatuma waangalizi wa uchaguzi kufuatilia zoezi la upigaji kura nchini Uganda.

Taarifa ya umoja huo imesema kuwa waangalizi hao watafuatilia kwa makini uchaguzi wa rais, wa bunge pamoja na wa serikali za mitaa na umeitaka serikali ya Kampala na wasimamizi wa uchaguzi kutoa ushirikiano kwa waangalizi hao.

Umoja wa Afrika umesema utatuma nchini Uganda timu ya watu 40 itakayoongozwa na Bi. Sofia Okofor kutoka mahakama ya kilele ya Ghana kuanzia hapo kesho na kwamba ujumbe huo utabakia Uganda hadi Februari 22. Waangalizi watafuatilia maandalizi ya kura na vilevile zoezi la kuhesabu kura na kutangazwa matokeo baada ya upigaji kura kumalizika.

Uchaguzi mkuu wa Uganda unatarajiwa kufanyika Februari 18 na kiti cha urais kimewavutia wagombea 8 akiwemo rais wa sasa, Yoweri Museveni. Hata hivyo mchuano mkali kwenye kiti cha urais unatarajiwa kuwa kati ya Bw. Museveni na Dktari Kizza Besigye wa chama cha FDC pamoja na Waziri Mkuu wa zamani, Amama Mbabazi ambaye anawania nafasi hiyo kama mgombea binafsi.