Algeria: Kadhia ya Palestina ipo ndani ya vipaumbele vyetu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i89962-algeria_kadhia_ya_palestina_ipo_ndani_ya_vipaumbele_vyetu
Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) katika mji mkuu Algiers, Rais wa Algeria ameitaja kadhia ya Palestina kuwa suala muhimu na nyeti.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 02, 2022 04:14 UTC
  • Algeria: Kadhia ya Palestina ipo ndani ya vipaumbele vyetu

Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) katika mji mkuu Algiers, Rais wa Algeria ameitaja kadhia ya Palestina kuwa suala muhimu na nyeti.

Algeria tangu awali imekuwa ikiunga mkono kadhia ya Palestina kwa kutetea haki za wananchi madhulumu wa Palestina na kuunga mkono malengo ya Quds kwa njia mbalimbali.  

Viongozi wa serikali ya Algeria aidha wamekuwa wakifuatilia matukio ya Quds Tukufu tangu kuanza mapigano kati ya raia wa Palestina na wanajeshi wa Kizayuni katika mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani; kupitia kufanya mawasiliano na uratibu na nchi nyingine za Kiarabu. 

Rais Abdel Majid Teboune wa Algeria amesema katika ufunguzi wa Mkutano wa 31 wa Viongozi wa Arab League huko Algiers mji mkuu wa nchi hiyo kwamba: suala nyeti na lenye umuhimu kwetu ni kupatikana haki za Wapalestina na kuundwa nchi huru ya Palestina mji mkuu wake ukiwa Quds Tukufu. 

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Rais wa Algeria amesema, migogoro inayoendelea Libya, Syria na Yemen inahitajia ufumbuzi. 

Mkutano wa 31 wa siku mbili wa Wakuu wa Nchi za Kiarabu umeanza tangu jana huko Algiers. Ajenda kuu za mkutano huo zinahusiana na masuala ya dharura ya kikanda ikiwemo hali ya mgogoro huko Yemen, Libya na Russia, kadhia ya Palestina na pia njia za kudhamini usalama wa chakula na kuimarisha uhusiano miongoni mwa nchi za Kiarabu.   

Mkutano wa 31 wa viongozi wa Arab League nchini Algeria