Wafungwa sita wa Zimbabwe watoroka kizuizini Afrika Kuisini, polisi inawasaka washukiwa
(last modified Tue, 14 Mar 2023 11:41:51 GMT )
Mar 14, 2023 11:41 UTC
  • Wafungwa sita wa Zimbabwe watoroka kizuizini Afrika Kuisini, polisi inawasaka washukiwa

Polisi ya Afrika Kusini imetangaza kuwa imeanzisha msako wa kuwasaka washukiwa "wenye silaha nzito" ambao wamewaachilia huru wafungwa sita katika mapigano makali ya risasi.

Raia sita wa Zimbabwe, wote wanaoshukiwa kuwa majambazi wakiwa na silaha, walitoroka kutoka kizuizini jana Jumatatu asubuhi baada ya wenzao kukabiliana na polisi wa Afrika Kusini katika majibizano ya risasi.

Shambulio hilo lilifanyika umbali wa kilomita 120 kusini mwa Beitbridge - mji wa mpakani karibu na Zimbabwe.

Taarifa iliyotolewa na Polisi ya Afrika Kusini imesema: "Watu wanashauriwa kutokaribia maeneo ya washukiwa hao kwa hali yoyote ile kwa sababu wanatambuliwa kuwa hatari, na badala yake watoe ripoti kwa polisi."

Zimbabwe ina idadi kubwa ya wahamiaji nchini Afrika Kusini na raia wake wanaendelea kukimbia matatizo ya kisiasa na kiuchumi nchini kwao.

Serikali ya Afrika Kusini imekuwa ikikabiliana na raia wa kigeni hasa Wazimbabwe wanaohusishwa na uhalifu wa kutumia mabavu.