Harakati ya Kiislamu Nigeria: Shekh Zakzaky agawa misaada ya chakula kwa wahitaji
Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imetangaza kuwa imegawa vifurushi mbaimbali bidhaa za chakula kwa watu wanohitajia nchini humo.
Harakati ya Kiislamu Nigeria imeeleza kuwa, harakati hiyo imegawa vifurushi vya chakula kwa watu wanaohitajia huko Nigeria katika kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Sheikh Ibrahim al-Zakzaky, kiongozi wa harakati ya Kiislamu ya Nigeria ndiye aliyeagiza kugawiwa misaada hiyo ya chakula kwa familia zenye uhitaji nchini Nigeria katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani.
Waislamu nchini Nigeria huupokea na kuukaribisha pakubwa mwezi Mtukufu wa Ramadhani kama ilivyo kwa Waislamu wengine duniani.
Waislamu katika nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika khususan vijana katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani husoma sana Qur'ani Tukufu na kujumuika pia misikitini ili kunufaika na tafsiri ya kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu.
Nigeria ni nchi iliyo na idadi kubwa ya watu barani Afrika na zaidi ya nusu ya watu wa nchi hiyo ni Waislamu. Nigeria aidha ni nchi iliyo na Waislamu wengi wa Kishia barani Afrika.