Wanaharakati wataka kukomeshwa ukiukwaji wa haki za binadamu Burundi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i9973-wanaharakati_wataka_kukomeshwa_ukiukwaji_wa_haki_za_binadamu_burundi
Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wameitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ishughulikie ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Burundi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 25, 2016 23:42 UTC
  • Wanaharakati wataka kukomeshwa ukiukwaji wa haki za binadamu Burundi

Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wameitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ishughulikie ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Burundi.

Marguerite Barankitse ambaye ni mtetezi wa haki za binadamu wa Burundi amesema ana waasiwasi kwamba, mgogoro wa ndani nchini humo unaweza kushadidi na kuwa mauaji ya kimbari.

Barankitse ambaye alikuwa akipokea tuzo ya Ulaya kwa juhudi zake za kibinadamu, amesema kuwa dunia nzima inajua vyema jinai zinazofanywa na Pierre Nkurunziza na kwamba jamii ya kimataifa inapaswa kumfikisha katika Kahakama ya Kimataifa ya Jinai.

Amesem kuwa zaidi ya watu elfu sita wanashikiliwa katika jela za Burundi na kwamba kumegunduliwa makaburi 9 ya umati ingawa hadi sasa hakuna takwimu kamili kuhusu watu waliopoteza maisha yao katika mgogoro wa sasa wa nchi hiyo.

Mwanaharakati huo wa haki za binadamu ametahadharisha kwamba, hali ya sasa na Burundi na kimya cha taasisi za kimataifa vinatia wasiwasi.

Burundi imetumbikia katika mgogoro mkubwa wa ndani na mauaji ya hapa na pale yamekuwa yakiripotiwa mara kwa mara nchini humo hususan baada ya Rais Pierre Nkurunziza kugombea tena kiti hicho licha ya upinzani mkubwa wa vyama vya siasa.