Raisi aondoka Kampala kuelekea ziarani Harare
(last modified Thu, 13 Jul 2023 08:10:11 GMT )
Jul 13, 2023 08:10 UTC
  • Raisi aondoka Kampala kuelekea ziarani Harare

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo Alhamisi ameondoka Kampala na kuelekea Harake mji mkuu wa Zimbabwe baada ya kukamilisha ziara huko Uganda.

Akiwa ziarani huko Uganda Rais Sayyid Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Yoweri Museveni wa nchi hiyo. Aidha jumbe za ngazi ya juu za nchi mbili zimesaini hati nne muhimu za ushirikiano kati ya nchi mbili. 

Kuzinduliwa ofisi ya uvumbuzi na teknolojia ya Iran huko Uganda, kutembelea shamba la kilimo la nje la Iran nchini humo kukutana na wanaharakati wa kiuchumi wa Iran na Uganda, na kushiriki katika mkutano wa mazungumzo ya dini mbalimbali katika Msikiti wa Taifa wa Kampala zilikuwa miongoni mwa ratiba ya ziara ya Rais wa Iran huko Uganda.  

Rais Raisi akikutana na Waislamu wa Uganda 

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa katika fremu ya ushirikiano wake na nchi za dunia Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitazami tu upande wa nchi za Ulaya, bali mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran unatilia mkazo  suala la kuwa na uhusiano na ushirikiano mwema na nchi za bara la Afrika na Asia pia. 

Soko kubwa la Afrika ni jukwaa linalofaa kuuzia bidhaa za Iran; na katika mazingira hayo bara la Afrika linapewa zingatio na nafasi maalumu katika sera za nje za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.