-
Upizani Zimbabwe: Rais Mnangagwa hana uhalali wa kuongoza
Oct 24, 2018 02:52Kiongozi wa chama cha upinzani cha MDC nchini Zimbabwe, Nelson Chamisa ametoa mwito wa kuundwa Mamlaka ya Kitaifa ya Mpito akisisitiza kuwa hiyo ndiyo njia pekee ya kuupatia ufumbuzi mgogoro kuhusu uhalali wa serikali ya Rais Emmerson Mnangagwa.
-
António Guterres asisitiza umuhimu wa kuimarishwa nafasi ya askari wa Umoja wa Mataifa katika kurejesha usalama nchini CAR
Oct 24, 2018 02:51Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres ameutaka umoja huo kuimarisha nafasi yake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
-
Amnesty: Watu 52 wameaga dunia wakiwa kizuizini Madagascar
Oct 23, 2018 13:30Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema watu 52 walifariki dunia katika mazingira ya kutatanisha wakiwa korokoroni wakisubiri kesi zao mwaka jana 2017 nchini Madagascar.
-
Nigeria yaweka amri ya kutotoka nje mjini Kaduna baada ya mapigano ya kikabila kuua watu 55
Oct 23, 2018 06:55Maafisa wa serikali ya Nigeria wametuma kikosi maalumu cha polisi katika jimbo la Kaduna la kaskazini mwa nchi hiyo na kutangaza amri ya masaa 24 ya kutotoka nje baada ya kutokea mapigano ya kikabila yaliyoua makumi ya watu.
-
Ethiopia yasaini makubaliano ya amani na kundi la waasi wa Ogaden
Oct 23, 2018 03:02Ethiopia imesema kuwa imesaini makubaliano ya amani na kundi lililokuwa likipigania kujitenga la Waasi wa Harakati ya Taifa ya Ukombozi wa Ogaden (ONLF) na hivyo kuhitimisha rasmi uasi uliodumu kwa zaidi ya miongo mitatu katika mkoa wa Somalia mashariki mwa nchi hiyo.
-
Algeria na Mauritania zakutana kuzungumzia Sahara Magharibi
Oct 23, 2018 03:02Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Algeria na Mauritania wameitisha kikao cha pamoja cha kujadili hatima ya Sahara Magharibi inayopigania uhuru wake kutoka kwa Morocco.
-
Genge moja la kigaidi lasambaratishwa nchini Tunisia
Oct 23, 2018 03:01Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tunisia imetangaza habari ya kusambaratishwa genge moja la kigaidi magharibi mwa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
-
Vikao vya Bunge la Afrika vyaanza mjini Kigali Rwanda + Sauti
Oct 22, 2018 17:02Bunge la Afrika limefungua kikao chake cha wiki mbili mjini Kigali Rwanda ambapo kwa muda wa wiki mbili wabunge wake watajadili mambo kadhaa kuhusu demokrasia,uongozi bora na kurahisisha mafungamano ya biashara baina ya waafrika wenyewe. Ni kikao kilichofunguliwa na Rais Paul Kagame wa Rwanda ambaye pia ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika.
-
Wimbi la wakimbizi wa Kongo laleta matatizo nchini Uganda + Sauti
Oct 22, 2018 16:58Idadi kubwa ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanazidi kumiminika katika nchi jirani ya Uganda na kusababisha matatizo mengi ya kuwahudumia. Kigozi Ismael na maelezo zaidi kutoka Kampala
-
Paul Biya atangazwa mshindi wa urais nchini Cameroon
Oct 22, 2018 15:51Pau Biya, kiongozi wa zamani zaidi barani Afrika ametangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika tarehe 7 mwezi huu wa Oktoba, kwa kupata asilimia 71 ya kura. Hayo yametangazwa na Baraza la Katiba la nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.