-
Jiji la Port Sudan lashambuliwa kwa ndege isiyo na rubani kwa siku ya tano mfululizo
May 08, 2025 07:14Jiji la Port Sudan, mashariki mwa Sudan, Alhamisi asubuhi limekumbwa na shambulio jipya la ndege isiyo na rubani (drone) kwa siku ya tano mfululizo, huku mapigano makali yakiendelea kati ya jeshi na waasi wa RSF.
-
Afrika Kusini Kuendesha Mkutano wa Kilele wa G20 kwa mafanikio hata bila uwepo wa Marekani
May 08, 2025 07:09Afrika Kusini itahakikisha Mkutano wa Kilele wa G20 unafanikiwa, iwe Marekani itahudhuria au la, amesema Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Paul Mashatile.
-
Serikali ya Tripoli yapinga kupelekwa Libya wahamiaji kutoka Marekani
May 08, 2025 03:36Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya imepinga vikali mpango wowote wa kupokea wahamiaji haramu waliofukuzwa kutoka Marekani.
-
Makamanda 11 wa ugaidi wauawa katika operesheni za jeshi la Nigeria
May 08, 2025 03:34Takriban vinara 11 wa magenge ya kigaidi nchini Nigeria wameuawa na vikosi vya serikali katika operesheni za kupambana na ugaidi katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika.
-
Uwanja wa Ndege wa Port Sudan kutoka Lango la Matumaini hadi Uwanja wa Vita. Je, jitihada za kutoa msaada zitaendelea?
May 08, 2025 02:22Sauti ya ving'ora inasikika kutoka mbali. Moshi mweusi unatanda angani kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Port Sudan. Umati mkubwa wa watu unakimbia kuelekea moja ya kambi za maficho za muda.
-
Nigeria yageukia Akili Mnemba (AI) ili kukabiliana na taarifa za uongo na kukuza lugha za ndani
May 07, 2025 22:52Huku Akili Mnemba (AI) ikiendelea kuhuhisha sekta ya viwanda kote duniani, Nigeria nchi iliyo na uchumi mkubwa zaidi barani Afrika imeamua kukumbatia kwa kasi wimbi hili la kiteknolojia.
-
Shambulio jingine la droni laripotiwa Port Sudan, pande hasimu zinaendelea kupigana
May 07, 2025 22:50Watu walioshuhudia jana Jumatano waliripoti kujiri shambulio jingine la ndege zisizo na rubani katika mji wa mashariki wa Sudan wa Port Sudan huku mapigano makali yakiendelea kati ya Jeshi la Taifa na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF).
-
Rais Ruto wa Kenya amsamehe mtu aliyemrushia kiatu Migori
May 07, 2025 09:07Rais William Ruto amemsamehe mtu aliyemrushia kiatu wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Kehancha, Kuria Magharibi, Kaunti ya Migori, siku ya Jumapili.
-
UNHCR: Wakimbizi wa Sudan wanaoingia Chad wanaongezeka
May 07, 2025 03:42Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR, limeelezea wasiwasi wake kuhusu ongezeko la wakimbizi wa Sudan wanaoingia katika nchi ya Chad.
-
Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, IGAD na Rais Salva Kiir wajadili hali ya Sudan Kusini
May 07, 2025 03:41Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amefanya mazungumzo kuhusu hali ya nchi hiyo na ujumbe wa Umoja wa Afrika na Mamlaka ya Maendeleo ya Kikanda (IGAD), ofisi ya rais wa Sudan Kusini ilirifu kupitia mtandao wa Facebook.