-
Bunge la Algeria laanza kujadili muswada wa kujinaisha ukoloni wa Ufaransa
Dec 21, 2025 05:42Bunge la Algeria jana lilifungua mjadala kuhusu rasimu ya sheria inayotaka kujinaisha utawala wa kikoloni wa Ufaransa nchini humo kati ya mwaka 1830 na 1962.
-
Lavrov: Kuimarishwa usalama ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya Afrika
Dec 21, 2025 04:16Sergei Lavrov Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa kuimarisha amani na usalama barani Afrika ni jambo muhimu ili kuhakikisha ustawi wa bara hilo na maendeleo endelevu, na ni kipengee muhimu katika kudumisha amani duniani.
-
Ufyatuaji risasi Afrika Kusini; watu wenye silaha waua 9 karibu na Johannesburg
Dec 21, 2025 04:13Watu waliokuwa na silaha, usiku wa kuamkia leo, wamefyatua risasi kiholela katika kitongoji kimoja karibu na Johannesburg nchini Afrika Kusini na kuua takriban watu 9 na kujeruhi wengine kadhaa.
-
Benin yamtia mbaroni waziri wa zamani wa ulinzi kwa jaribio la mapinduzi lililoshindwa
Dec 20, 2025 23:08Benin, jana Jumamosi, ilimuweka kizuizini waziri wa zamani wa ulinzi na kiongozi wa upinzani, Candide Azannai, kama sehemu ya uchunguzi kuhusu jaribio la mapinduzi lililoshindwa mapema mwezi huu.
-
Mjumbe wa UN: Hali ya usalama bado ni tete katika mji mkuu wa Libya,Tripoli
Dec 20, 2025 23:06Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya Libya amesema kuwa hali ya usalama huko Tripoli imeboreka kwa kiasi fulani kufuatia mipango mipya ya usalama, hata hivyo ametahadharisha kuwa ukosefu wa usalama unaendelea kushuhudiwa katika mji huo mkuu na katika mikoa ya magharibi mwa Libya.
-
Viongozi wa Kiafrika wahimizwa kudumisha 'ujasiri' katika kushinikiza fidia ya utumwa
Dec 20, 2025 10:40Rais wa Ghana, John Dramani Mahama, amekutana na kuzungumza wajumbe wa kimataifa, lengo likiwa ni kutafuta fidia ya utumwa na ukoloni wa Wazungu katika maeneo mbalimbali ya dunia hasa barani Afrika.
-
Wanamgambo wa RSF wamewaachia huru wafanyakazi 9 wa sekta ya afya huko Darfur
Dec 20, 2025 10:33Mtandao wa Madktari nchini Sudan umeripoti kuwa wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) umewaachia huru wafanyakazi 9 wa sekta ya afya waliokuwa wakishikiliwa katika magareza na kikosi hicho huko Nyala makao makuu ya jimbo la Darfur Kusini. Hata hivyo kikosi cha RSF bado kinawashikilia wafanyakazi wengine wa afya 73.
-
Muda wa kuhudumu askari wa UN nchini DRC waongezwa huku waasi wakishadidisha vita
Dec 20, 2025 03:43Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja jana Desemba 19, 2025 limepitisha azimio namba 2808 (2025), ambalo linaamua kuongeza hadi tarehe 20 Desemba 2026 muda wa kazi wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (MONUSCO), na kwa hali ya kipekee, wa brigedi yake ya kukabiliana mashambulizi.
-
Rais Museveni: Tuna risasi za kutosha kukabiliana na wanaopanga kuandamana
Dec 20, 2025 00:33Rais Yoweri Museveni wa Uganda amewaonya wale wanaopanga kuandamana na kueleza kwamba, kuna risasi za kutosha kwa ajili ya kukabiliana nao.
-
Mashambulizi ya RSF yaua raia 16 eneo la Kordofan, Sudan
Dec 19, 2025 23:07Takriban watu 16 wameuawa katika shambulio la mizinga la waasi wa RSF lililolenga mji uliozingirwa katika eneo la Kordofan nchini Sudan, huku vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo vikiingia katika awamu hasasi kwenye mwaka wake wa tatu.