-
Mauaji yaongezeka Western Cape hasa Cape Town, nchini Afrika Kusini
Dec 19, 2025 07:19Takwimu za hivi karibuni zaidi za vitendo vya uhalifu nchini Afrika Kusini zinaonesha kuwa zaidi ya watu 1,000 waliuawa katika Mkoa wa Western Cape kati ya mwezi Julai na Septemba mwaka huu, huku Cape Town ikiwa kitovu cha vitendo vya uhalifu na vurugu katika eneo hil.
-
Mvurugiko wa hali ya hewa, Morocco yakumbwa na mawimbi ya baridi kali
Dec 19, 2025 07:18Katika kile kinachoonekana wazi kuwa ni madhara ya uchafuzi wa mazingira na mvurugiko wa hali ya hewa kutokana na uharibifu mkubwa wa hewa unaofanywa na madola ya viwanda duniani, taarifa kutoka Morocco zinasema kuwa, nchi hiyo ya jangwa imekumbwa na mawimbi makubwa ya baridi kali ambayo hayajawahi kutokea.
-
Rais wa Zambia aidhinisha sheria ya kupanua Bunge miezi kadhaa kabla ya uchaguzi
Dec 19, 2025 03:15Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema, jana Alkhamisi alisaini sheria ambayo itapanua Bunge la nchi hiyo, hatua ambayo wakosoaji wanasema inaweza kukinufaisha chama chake, miezi minane kabla ya uchaguzi wa kitaifa.
-
Jenerali Mkuu wa Sudan akutana na Rais wa Misri, vita vinaendelea
Dec 19, 2025 07:19Jenerali Mkuu wa Sudan, Abdel-Fattah al Burhan, amekutana na Rais wa Misri, Abdel-Fattah el-Sissi mjini Cairo huku kukiwa na shinikizo linalozidi kuongezeka la kuhimiza kutatuliwa mgogoro wa vita nchini Sudan haraka iwezekanavyo.
-
UN: Zaidi ya raia 1,000 waliuawa katika shambulio la RSF Darfur
Dec 18, 2025 08:22Ripoti iliyotolewa Alkhamisi na Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema zaidi ya raia 1,000 waliuawa wakati kundi la waasi wa Sudan lilipotwaa udhibiti wa kambi ya wakimbizi wa ndani huko Darfur nchini Sudan mwezi Aprili mwaka huu.
-
Waasi wa M23 wamebaki Uvira licha ya kutangaza kuwa tayari kuondoka katika mji huo
Dec 18, 2025 03:55Waasi wa kundi la M23 hawajaondoka katika mji wa Uvira mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo licha ya mapema wiki hii kutangaza kuwa wataondoka katika mji huo.
-
Watu wasiopungua 12 wauawa katika shambulizi kwenye eneo la uchimbaji madini huko Plateau, Nigeria
Dec 18, 2025 03:54Takriban watu 12 wameuawa na wengine watatu kutekwa nyara baada ya watu wenye silaha kushambulia eneo la uchimbaji madini katika kijiji cha Atoso katika jimbo la Plateau nchini Nigeria.
-
Wabangladesh 32 waokolewa katika maji ya Libya
Dec 17, 2025 23:18Wahamiaji thelathini na wawili wa Bangladesh wameokolewa baada ya boti yao kuzama katika pwani ya mji wa Al-Haniya wa kaskazini mashariki mwa Libya.
-
A/Kusini yavamia kituo cha wakimbizi cha Marekani, yakamata Wakenya saba
Dec 17, 2025 23:18Kituo kimoja nchini Afrika Kusini kinachoshughulikia maombi ya visa za Marekani kimevamiwa na maafisa wa uhamiaji wa Afrika Kusini na kuwatia mbaroni raia saba wa Kenya waliokuwa wanafanya kazi nchini humo kinyume cha sheria.
-
Je, mashinikizo ya Marekani yameufanya mchakato wa uteuzi wa Waziri Mkuu nchini Iraq kuwa tata zaidi?
Dec 17, 2025 23:10Gazeti la Al-Akhbar limeandika katika ripoti yake kwamba, kuongezeka kwa mashinikizo ya kisiasa ya Marekani dhidi ya Baghdad kumeufanya mchakato wa kuunda serikali mpya ya Iraq kuwa tata zaidi.