-
Wasiwasi wa Russia kuhusu kusambaa zaidi ugaidi kutokea Afghanistan
Apr 28, 2024 23:05Waziri wa Ulinzi wa Russia ametangaza kuwa tishio kuu kwa Asia ya Kati ni kutoka kwa makundi ya kigaidi yenye misimamo mikali yenye makao makuu nchini Afghanistan.
-
Kushadidi mgogoro wa kisiasa katika baraza la mawaziri la utawala wa Kizayuni
Apr 28, 2024 07:22Kuendelea maandamano ya mitaani huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel), tofauti za kimtazamo kati ya wapinzani na baraza la mawaziri na kuongezeka uwezekano wa Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu kutoa amri ya kumkamata Benjamin Netanyahu kumezidisha mzozo wa kisiasa huko Tel Aviv.
-
UN yaunga mkono maandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu Marekani ya kuwatetea watu wa Gaza
Apr 28, 2024 00:56Stephen Dujaric Msemaji wa Umoja wa Mataifa jana Ijumaa alisema katika radiamali yake kwa maandamano yanayoendelea kufanywa na wanafunzi wa vyuo vikuu huko Marekani katika kuwaunga mkono watu wa Gaza na kupinga mauaji ya kimbari dhidi ya wakazi wa eneo hilo kwamba: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ni mfuasi na mungaji mkono mkubwa wa uhuru wa kujieleza, ikiwa ni pamoja na huko Marekani; na anaunga mkono haki ya wananchi ya kufanya maandamano kwa amani.
-
Iran Expo 2024, maonyesho ya uwezo wa kiuchumi wa Iran
Apr 27, 2024 07:13Maonesho ya sita ya uwezo wa kusafirisha nje bidhaa za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRAN EXPO 2024) yameanza leo mjini Tehran kwa lengo la kuonesha uwezo wa kiuchumi wa Iran.
-
Ukosoaji wa Amnesty International kwa njama za Marekani za kuficha jinai za Israel Gaza
Apr 26, 2024 23:05Agnes Callamard, Katibu Mkuu wa Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International, ameonya kuhusu kuendelea kwa ukiukaji wa haki za binadamu huko Gaza na kutangaza kuwa: Marekani inazuia kutuhumiwa Israel kwa kukiuka haki za binadamu katika Ukanda wa Gaza.
-
Kikao cha Pili cha Kimataifa cha Iran na Afrika; nembo ya azma ya kupanua ushirikiano
Apr 26, 2024 11:07Kikao cha pili cha kimataifa kati ya Iran na Afrika kimefanyika leo asubuhi (Ijumaa) kwa kuhudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu wa masuala ya kiuchumi wa nchi zaidi ya 30 za Afrika na kwa hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika ukumbi wa mikutano wa nchi za Kiislamu mjini Tehran.
-
Marekani yashadidisha ukandamizaji dhidi ya wapinzani wa utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wa Palestina
Apr 25, 2024 23:39Marekani ndiyo muungaji mkono mkubwa zaidi wa utawala wa Kizayuni wa Israel ambapo serikali ya Biden imetoa msaada mkubwa zaidi wa kijeshi na silaha kwa Tel Aviv wakati wa vita vya Gaza, ambavyo vimeingia katika mwezi wake wa saba.
-
Ushauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi kuhusu kutumia vikwazo kama fursa ya maendeleo
Apr 25, 2024 07:47Akiashiria nafasi muhimu ya jumuiya ya wafanyakazi katika kuongeza uzalishaji na kuboresha hali ya kiuchumi ya Iran, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameyataja maendeleo ya Jamhuri ya Kiislamu katika sekta mbalimbali hususan silaha kuwa ni mfano wa kugeuza vikwazo kuwa fursa.
-
Kuiwekea vikwazo sekta ya ulinzi ya Iran, zawadi mpya iliyotunukiwa Israel na Magharibi
Apr 24, 2024 23:05Katika hatua uliyochukua ili kuufurahisha utawala wa Kizayuni wa Israel, Umoja wa Ulaya umetangaza kuwa utapanua wigo wa vikwazo ulivyoiwekea sekta ya ulinzi ya Iran.
-
Sisitizo la Rais wa Iran kwamba Palestina ni suala kuu la Ulimwengu wa Wanadamu
Apr 24, 2024 03:49Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kwa mara nyingine tena kuwa kadhia ya Palestina ndilo suala kuu la Ulimwengu wa Wanadamu.