Kwa mara nyingine rais kizee wa Marekani achapa usingizi mbele ya kamera barani Afrika + VIDEO
https://parstoday.ir/sw/news/event-i119756
Kwa mara nyingine dunia imeshuhudia jinsi rais kizee wa Marekani anavyoazirika mbele ya kamera za kimataifa wakati alipoonekana akichapa usingizi na baadaye kujifanya kama hakusinzia.
(last modified 2025-06-15T08:05:10+00:00 )
Dec 06, 2024 02:33 UTC
  • Kwa mara nyingine rais kizee wa Marekani achapa usingizi mbele ya kamera barani Afrika + VIDEO

Kwa mara nyingine dunia imeshuhudia jinsi rais kizee wa Marekani anavyoazirika mbele ya kamera za kimataifa wakati alipoonekana akichapa usingizi na baadaye kujifanya kama hakusinzia.

Tukio hilo limetokea kwenye mkutano muhimu wa kiuchumi kati yake na viongozi wa Afrika wakati wa ziara yake ya siku tatu barani humo. Picha zinazomuonesha rais huyo kizee wa Marekani akichapa usingizi zimeenea sana katika mitandao ya kijamii. 

Biden ametembelea nchi ya Angola katika safari yake barani Afrika ikiwa imebakia kipindi cha chini ya miezi miwili kabla ya kuondoka madarakani huko Marekani.

Mkanda huu wa video unamuonesha rais huyo wa Marekani akichapa usingizi akiwa kwenye meza kuu ya mazungumzo na viongozi wa Afrika na wakati mmoja wa viongozi wa Afrika alipokuwa anahutubia.

 

Biden alijaribu kuziba uso wake kwa mikono yake na kujifanya hajalala lakini usingizi unamzidi nguvu na ujanja wake haukuzuia kamera kumchukua akiwa amelala mpaka mkono wake kutikisika kwa usingizi mzito. 

Wananchi wa Marekani wanashangaa kuona picha hizo na wengine wanauliza "ni nani anayeongoza Marekani?"

Mkutano huo ulifanyika katika mji wa bandari wa Lobito nchini Angola juzi Jumatano ili kujadili mpango wa kupanua njia ya reli itakayoweza kusafirisha madini muhimu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Zambia hadi kwenye bandari hiyo ya Lobito ya Angola na baadaye kupelekewa nchi za Magharibi. Biden amekwenda Angola kujaribu kupunguza ushawishi wa China lakini kamera zimemchukua akichapa usingizi kwenye mkutano huo muhimu sana.