-
Mkuu wa Jeshi la Polisi la Tanzania atembelea eneo walipouliwa Watanzania + Sauti
Jun 30, 2019 12:40Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania (IGP), Simon Sirro amesema imebainika kuwa waliowaua Watanzania 9 kwa kuwapiga risasi na wengine kushambuliwa kwa mapanga ambao ni watu wasiojulikana, walianza chokochoko hizo katika eneo la Kibiti mkoani Pwani baada ya kutimuliwa na na Jeshi la Polisi la Tanzania na wengine wakakimbilia nchi jirani ikiwemo Msumbiji. Maelezo zaidi yamo katika ripoti ya mwandishi wetu wa Dar es Salaam, Ammar Dachi.
-
Mbunge 'Jaguar' anyimwa dhamana nchini Kenya + Sauti
Jun 28, 2019 12:43Mahakama nchini Kenya imemnyima dhamana, Mbunge wa eneobunge la Starehe jijini Nairobi Charles Njagua maarufu kwa jina la ‘Jaguar’ ambaye alikamatwa hivi karibuni na jeshi la polisi la nchi hiyo baada ya kutoa kauli ya kibaguzi dhidi ya Watanzania, Wachina na Waganda wanaoishi katika nchini hiyo mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mbunge huyo atasalia korokoroni hadi pale kesi yake itakaposikilizwa tena. Mwandishi wetu wa Mombasa, Kenya Seifullah Murtadha ana maelezo zaidi......
-
Matukio ya ulimwengu wa Kiislamu na Harith Subeit + Sauti
Jun 28, 2019 11:24Kama kawaida, wiki hii pia kuna matukio mengi ya Kiislamu yametokea katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki. Mwandishi wetu wa Zanzibar, Harith Subeit ametukusanyia baadhi ya matukio hayo katika ripoti yake hii ya kila wiki...
-
Makumi ya watu waaga dunia kwenye mgodi Kongo DR + Sauti
Jun 28, 2019 11:01Makumi ya wachimba migodi wamefariki dunia baada ya kuporomokewa na udongo kwenye mgodi wa shaba nyekundu na kobalti huko kusini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Kamati ya Mshikamano wa Wakenya na Wapalestina: Muamala ya Karne utagonga mwamba
Jun 27, 2019 12:29Vuguvugu la mshikamano baina ya Wakenya na Wapelestina limekosoa vikali kimya cha jamii ya kimataifa mbele ya ukandamizaji wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.
-
Polisi wawashikilia watuhumiwa 10 utekaji watu Rwanda + Sauti
Jun 27, 2019 04:29Polisi mjini Kigali Rwanda inawashikilia watu kumi na saba wakiwemo Wanyarwanda 15 na Wakenya wawili kwa shutuma za kuwatapeli vijana zaidi ya elfu tatu wakiwaahidi ajira hewa za ujasiriamali. Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera anaripoti zaidi...
-
SAUTI, Kazi ya ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme kwenye maporomoko ya Rusumo karibu itakamilika
Jun 24, 2019 13:36Nchi za Rwanda, Tanzania na Burundi zimetangaza kwamba kazi ya kuzalisha umeme kwenye maporomoko ya mto Rusumo iko mbioni kukamilika.
-
SAUTI, Mashirika matatu ya kujitegemea Burundi yalijia juu Shirika la Human Right Watch, yasema Burundi hali ni salama
Jun 24, 2019 13:30Mashirika matatu yasiyokuwa ya kiserikali nchini Burundi yameipinga ripoti ya Shirika la Kutetea Haki za Binaadamu la Human Rights Watch iliyosema kuwa, bado kunaendelea hali ya ukandamizaji na ukiukaji mkubwa wa haki za binaadamu nchini humo.
-
Mapigano ya kikabila DRC yazitia hofu asasi za kijamii + Sauti
Jun 19, 2019 22:06Asasi za kijamii za jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimekumbwa na wasiwasi baada ya kuzorota hali ya usalama katika mkoa wa Ituri wa kaskazini mwa nchi hiyo kutokana na mapigano ya kikabila yanayoendelea. Mossi Mwasi na maelezo zaidi kutoka Brazzaville.
-
Muungano vamizi wachoma moto kijiji kizima Yemen + Video, Picha
Jun 16, 2019 06:28Mamluki wa Saudi Arabia wamechoma moto kijiji kizima katika mkoa wa al Hudaida nchini Yemen na kuongeza orodha ya jinai zao dhidi ya wananchi madhlumu wa Yemen, baada ya wavamizi hao kushindwa katika medani za kivita.