May 26, 2024 04:42 UTC
  • Kusifiwa kimataifa Shahidi Ebrahim Raisi

Tarehe 30 mwezi huu wa Mei, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) litafanya marasimu ya kuenzi na kumkumbuka marehemu Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri wa Kiislamu Iran aliyekufa shahidi akiwa na viongozi wengine wa ngazi za juu kitaifa, katika ajali ya helikopta iliyotokea katika eneo la kaskazini magharibi mwa nchi.

Dennis Francis, Mwakilishi wa Trinidad na Tobago ambaye ni mwenyekiti wa sasa wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa alitangaza suala hilo katika barua aliyowatumia wawakilishi na waangalizi wote wa kudumu wa nchi zao katika Umoja huo. Mwenyekiti huyo wa awamu ya 78 ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa alifika katika Ofisi ya Uwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika taasisi hiyo ya Kimataifa mjini New York na kutoa heshima zake za mwisho kwa Shahidi Ebrahim Raisi na waziri wake wa mambo ya nje Hussein Amir-Abdollahian kwa kutia saini kitabu cha kumbukumbu cha kidiplomasia kwa ajili ya kuwaenzi shakhsia wawili hao walioaga dunia wakiwa na wenzao katika ajali hiyo ya ndege.

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa alisema katika hotuba yake kwenye mkutano wa Baraza Kuu: Ni wajibu wangu kuenzi kumbukumbu ya Marehemu Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambaye kwa bahati mbaya aliaga dunia tarehe 19 Mei 2024.

Awali, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikuwa limenyamaza kimya kwa dakika moja kwa heshima ya rais na waziri wa mambo ya nje wa Iran walioaga shahidi na wenzao katika ajali hiyo ya helikopta, na bendera ya Umoja wa Mataifa pia ilishushwa nusu mlingoti.

Kadhalika, hadi sasa mabalozi na wawakilishi wa zaidi ya nchi 50 wametoa heshima zao kwa Rais Ebrahim Raisi, aliyekufa shahidi na wenzake Jumapili iliyopita katika ajali ya helikopta, kwa kutia saini kitabu cha kumbukumbu katika Ofisi ya Uwakilishi ya Iran katika Umoja wa Mataifa.
Wakati huo huo wakuu na maafisa wakuu wa nchi na asasi za kieneo na kimataifa wapatao 90 wametoa heshima zao kwa shahidi Ayatullah Raisi na mashahidi wengine wa ajali hiyo kwa kuhudhuria mazishi  ya mashahidi hao katika Ukumbi wa Kikao cha Viongozi mjini Tehran.

Suala hilo linaonyesha wazi kuwa huduma kubwa aliyoitoa Shahidi Ebrahim Raisi haikuhisika ndani ya nchi na kwa watu wa Iran pekee, bali taasisi na watu wengi katika jumuiya ya kimataifa pia wanathamini juhudi zake kubwa alizofanywa katika ngazi za kimataifa kwa lengo la kutatua matatizo yanayoikabili jamii ya mwanadamu wa sasa.

Shahidi Ebrahim Raisi aliingia katika medani ya uchaguzi wa rais wa Iran kwa lengo la kuwatumikia waja wa Mwenyezi Mungu, na kwa kutilia maanani utambuzi na uzoefu ambao wananchi walikuwa wameupata kutoka kwake alipohudumu katika nyadhifa mbalimbali, hususani katika kipindi cha uongozi wake katika mji mtakatifu wa Mashhad, wakaamua kumchagua kuwa rais wao.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran baada ya kuchukua uongozi wa serikali alitoa mchango mkubwa katika kutatua matatizo ya wananchi wa Iran na hasa ya kiuchumi na kupambana na ufisadi serikalini.

Iran yaomboleza kifo cha shahidi Ebrahim Raisi

Moja ya sifa zake za kuvutia ilikuwa urafiki wake na watu katika safari zake za mikoani, ambapo aliona na kusikia shida za watu kwa karibu  na kufikiria njia za kuzitatua.
Shahidi Sayyid Ebrahim Raisi, aliamini moyoni mwake kwamba kuwatumikia waja wa Mwenyezi Mungu ni ibada, kwa hiyo hakusalimu amri mbele ya machovu na matatizo bali aliamua kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kupata radhi za Mwenyezi Mungu na wakati huo huo kufurahisha mioyo ya watu.
Kupunguza umaskini, kurahisisha maisha ya watu na kuwapatia makazi ni miongoni mwa kero kuu zilizomshughulisha marehemu shahidi Ebrahim Raisi, ambaye licha ya vikwazo vya nchi za Magharibi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran lakini alitekeleza vizuri kazi hiyo.

Alikarabati miundombinu ya kiuchumi na kuunga mkono kwa pande zote uzalishaji wa ndani.

Serikali ya shahidi Rais Ebrahim Raisi, pia ilifuata diplomasia amilifu kieneo na kimataifa ambapo alitumia fursa za kikanda kimataifa kwa maslahi ya taifa la Iran.

Kujenga uaminifu kati ya nchi jirani na za kikanda, kupunguza mivutano na kuangazia nguvu ya kieneo ni miongoni mwa mafanikio muhimu ya serikali ya shahidi Rais Ebrahim Raisi..

Nchi za Amerika ya Latini na Afrika zinachukuliwa kuwa sehemu ya marafiki na washirika wa Jamhuri ua Kiislamu ya Iran na mwingiliano huo ni zaidi ya mahusiano ya kisiasa tu.

Kuendelea kuheshimiwa Rais Sayyid Ebrahim Raisi katika ngazi za kimataifa kunaonyesha wazi kwamba jamii nyingi za dunia pia zinahisi pengo kubwa ambalo limeachwa naye kutokana na huduma zake muhimu katika kuimarisha amani na utulivu wa kimataifa kwa maslahi ya jamii ya mwanadamu.