Oct 07, 2024 07:24 UTC
  • Rais Pezeshkian: Iran inakaribisha mazungumzo na Ulaya ili kuimarisha uhusiano

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, taifa hili linakaribisha mazungumzo na nchi za Ulaya kwa ajili ya kutatua masuala na kuimarisha uhusiano.

Rais Masoud Pezeshkian amesema hayo katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Waziri Mkuu wa Uholanzi Dick Schoof. Rais wa Iran akizungumzia historia ya miaka 400 ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili, amesema, Iran inataka kutatua baadhi ya masuala kama vile suala la nyuklia kwa njia ya mazungumzo na kuimarisha uhusiano na ushirikiano wake na majirani zake na nchi nyingine za dunia, zikiwemo nchi za Ulaya.

Pezeshkian amesema, utawala haramu wa Israel uukiwa na lengo la kufidia kushindwa kwake katika Ukanda wa Gaza na kueneza mvutano na migogoro katika eneo, ulimuua mgeni rasmi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Tehran yaani Ismail Haniyeh na nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani badala ya kulaani, jinai na vitendo vya kigaidi vya Wazayuni, mara kwa mara waliiomba Iran ijizuie na kushikamana na subira.

Kwa uupande wake Waziri Mkuu wa Uholanzi ameeleza kuwa, nchi hii inakaribisha utendaji wa serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kupanua uhusiano na nchi za Ulaya, na akataka hatua madhubuti zichukuliwe kuhusiana na suala hilo.