Baada ya Wazayuni kueneza uvumi wa kipuuzi, hatimaye Jenerali Qaani ajitokeza hadharani
(last modified Tue, 15 Oct 2024 06:23:20 GMT )
Oct 15, 2024 06:23 UTC
  • Baada ya Wazayuni kueneza uvumi wa kipuuzi, hatimaye Jenerali Qaani ajitokeza hadharani

Brigedia Jenerali Ismael Qaani, Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran SEPAH ameonekana hadharani katika mazishi ya Shahhid Abbas Nilforoushan na kubatilisha njama na uvumi wote wa Wazayuni dhidi ya Jenerali Qaani.

Kwa mujibu wa shirika la habari la FARS, mwili wa shahid Abbas Nilforoushan ambaye aliuawa kidhulma kwenye shambulio la kigaidi na kikatili lililofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel huko Beirut, mji mkuu wa Lebanon, umewasili usiku wa kuamkia leo Jumanne hapa Tehran.

Brigedia Jenerali Ismael Qaani, Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ameonekana akiwa kwenye kikao cha maombolezo kilichohudhuriwa na wakuu mbalimbali za kisiasa na kijeshi, watu wa familia ya shahid Nilforoushan na kadhalika.

Shahid Abbas Nilforoushan

 

Shahid Nilforoushan aliuawa kikatili tarehe 27 Septemba 2024, kusini mwa Beirut, mji mkuu wa Lebanon akiwa pamoja na Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa harakati ya mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya nchi hiyo.

Shahid Nilforoushan alikuwa mmoja wa shakhsia na makamanda muhimu sana wa Iran aliyeongoza operesheni nyingi za kuwasaidia Walebanon na Wapalestina katika kupambana na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Aliisaidia sana kambi ya Muqawama katika mipango ya kijeshi na kidiplomasia na namna ya kukabiliana na jinai za Israel ndio maana utawala wa Kizayuni ulikuwa na chuki na uadui mkubwa na mwanamapambano huyo wa Kiislamu.