Meja Jenerali Salami: Adui anaporomoka; Muqawama utaibuka na ushindi
(last modified Fri, 03 Jan 2025 03:44:44 GMT )
Jan 03, 2025 03:44 UTC
  • Meja Jenerali Salami: Adui anaporomoka; Muqawama utaibuka na ushindi

Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesisitiza kuwa, vita vya kisaikolojia vya adui Mzayuni ni ishara ya mwisho wake, na Muqawama utaibuka na ushindi.

Akizungumza pembezoni mwa shughuli ya kumbukumbu ya mauaji ya Shahid Qassem Soleimani katika Huseiniya ya Imam Khomeini mjini Tehran, Meja Jenerali Hossein Salami, Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, amewahutubia vijana wa Mhimili wa Muqawama akisema: Kwa vijana wote wa Mhimili wa Muqawama nchini Iraq, Yemen, Lebanon na kwingineko, natangaza kwamba adui anazidi kudidimia na kuporomoka, na operesheni ya vita vya kisaikolojia ambayo adui anaifanya inaonyesha mwisho wa kazi yake na kuporomoka.

Kamanda Salami ameongeza kuwa, kama alivyosisitiza Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei, Muqawama utapata ushindi na tutapata mafanikio na ushindi kwa Muqawama na kusimama kidete.

Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza pia kuwa: Utawala wa Kizayuni wa Israel umeshindwa kukabiliana na uwezo wa makombora wa vikosi vya Ansarullah ya Yemen, ambavyo ni sehemu ya Mhimili wa Muqawama, na Mwenyezi Mungu akipenda, hatimaye Muqawama utapata ushinda.