Rais Pezeshkian: Jibu halali na kali la Iran litamfanya adui kujuta
Katika ujumbe wake kwa taifa kufuatia jinai ya kinyama iliyofanywa na utawala wa Kizayuni usiku wa kumkia leo, Rais Masoud Pezeshkian amesisitiza juu ya ulazima wa watu kujiepusha na uvumi katika vita vya kisaikolojia vya adui na kuwaunga mkono na kuwaamini viongozi na kusema: Taifa la Iran na maafisa wa nchi hawatonyamaza mbele ya jinai hiyo.
Akisisitiza kwamba jibu halali na kali la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran litamfanya adui ajutie kitendo chake cha kipumbavu, Rais Pezeshkian amesema, leo taifa la Iran linahitaji umoja, uaminifu, uelewano, umoja na maafikiano kuliko wakati mwingine wowote, na kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, kwa moyo huo wa thamani, litatoa jibu kali, la busara na kali kwa jinai ya utawala unaoikalia kwa mabavu Quds."
Sehemu moja ya ujumbe wake inasema: Uchokozi wa usiku wa kuamkia leo umewathibitishia walimwengu wote uhalali wa madai ya muda mrefu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwamba uchokozi na jinai ni asili katika dhati na maumbile ya utawala wa Kizayuni. Bila shaka taifa la Iran na maafisa wa nchi hawatanyamaza kimya mbele ya jinai hiyo, na jibu halali na kali la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran litamfanya adui ajutie hatua yake hiyo ya kipumbavu.
Awali katika taarifa ya kulaani shambulio lililofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya ardhi tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mapema leo alfajiri, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, alitoa ujumbe mzito kwa taifa la Iran, akisisitiza kuwa adhabu kali inamsubiri mhalifu huyo wa kimataifa.
Ayatullah Khamenei alisema kuwa mashambulizi hayo ya alfajiri yaliyolenga maeneo ya raia, yamedhihirisha kwa mara nyingine asili ya kikatili ya utawala wa Kizayuni.