Haj Ali Akbari: Hatutahadaika na mchezo wa Snapback
Khatibu wa muda wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran amesema kuhusiana na kuhuishwa utaratibu wa "Snapback" kwamba: Inapasa kuzingatiwa kuwa baada ya kuvuka vikwazo vinavyolemaza; masuala haya kwa kiasi kikubwa ni ya kisaikolojia na ni hila yenye lengo la kupotosha fikra za waliowengi, na kamwe Iran haiwezi kuhadaika na michezo hii.
Hujatul Islam Wal Muslimin Muhammad Javad Haj Ali Akbari amesema katika hotuba za Sala ya Ijumaa ya leo katika Chuo Kikuu cha Tehran kwamba: Tunashuhudia hatua nzuri sana zikichukuliwa katika uga wa diplomasia na tunawashukuru kwa dhati viongozi wote, hasa Mheshimiwa Rais, Waziri wa Mambo ya Nje, pamoja na Baraza Kuu la Usalama wa Taifa na Katibu wake.
Amesema: Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa maelewano imeasisiwa harakati iliyoratibiwa yenye mshikamano na nguvu kubwa. Tunatumai kuwa mwenendo huu utaendelea hasa katika mazungumzo na mijadala kwa umakini na tahadhari kubwa.
Khatibu wa muda wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran ameeleza kuwa: Kuhusu mchezo wa "Snapback" na kadhia nyingine zinazofanana na hizo; Pamoja na kuwa chombo cha diplomasia cha Iran kinafanya kazi ipasavyo lakini inapasa kutiliwa maanani kuwa baada ya kuvuka vikwazo vyenye kulemeza suala hili kwa kiasi kikubwa ni la kisaikolojia na ni hila yenye lengo la kupotosha fikra za waliowengi. Iran kamwe haitahadaiwa na michezo hii.
Haj Ali Akbari ameongeza kuwa: Kama alivyoeleza Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi; anga ya sasa sio vita wala amani bali ni fursa kwa ajili ya kazi, ubunifu na kutegemea uwezo wa ndani. Somo muhimu tulilojifunza kutoka kujihami kutakatifu kwa mara ya kwanza na ya pili ni kujiamini na kutegemea uwezo na nguvu za ndani. Hadi leo pia tumestafidi na njia hii kwa kuwaamini vijana na vipaji vikubwa vya kizazi cha vijana wa nchi hii. Kwa ari hii, tunaweza kuendelea na njia hii kwa nguvu na azma kubwa kuliko ilivyokuwa huko nyuma.