Iran kuzindua satelaiti 3 mwanzoni mwa msimu wa baridi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i133044-iran_kuzindua_satelaiti_3_mwanzoni_mwa_msimu_wa_baridi
Hassan Salarieh, mkuu wa Shirika la Anga za Juu la Iran (ISA) ametangaza mipango ya kurusha kwenye obiti satelaiti tatu zilizoundwa hapa nchini kama sehemu ya jitihada za kuboresha mpango wa anga za juu wa nchi.
(last modified 2025-11-11T07:46:58+00:00 )
Nov 11, 2025 07:46 UTC
  • Iran kuzindua satelaiti 3 mpya
    Iran kuzindua satelaiti 3 mpya

Hassan Salarieh, mkuu wa Shirika la Anga za Juu la Iran (ISA) ametangaza mipango ya kurusha kwenye obiti satelaiti tatu zilizoundwa hapa nchini kama sehemu ya jitihada za kuboresha mpango wa anga za juu wa nchi.

Satelaiti hizo tatu kwa majina ya Zafar, Paya na Kowsar zitazinduliwa mwanzoni mwa msimu wa baridi mwaka huu. Satelaiti hizo zinafanyiwa maandalizi ya mwisho ya kiufundi, na tarehe ya kuzinduliwa itatangazwa hivi karibuni.

Satelaiti za Zafar, Paya, na Kowsar zimetengenezwa na wahandisi wa Kiirani chini ya makampuni mbalimbali kwa ushirikiano na Shirika la Anga za Juu la Iran (ISA).

Zafar ni satelaiti ya hali ya juu ya uchunguzi iliyotengenezwa ili kutoa taswira ya mwonekano wa juu kwa matumizi muhimu katika kilimo, ufuatiliaji wa mazingira na udhibiti wa maafa.

Paya, kama ilivyo Zafar, ni satelaiti ya uchunguzi iliyotengenezwa kwa ajili ya upigaji picha wa hali ya juu na ukusanyaji wa data za hali ya juuu.

Kowsar imeundwa kwa ajili ya upigaji picha wa ubora wa juu kwa kuzingatia kilimo sahihi. Itatoa picha za kila siku za mimea ya kijani kibichi, ikisaidia ufuatiliaji wa kilimo, tathmini ya afya ya mazao na usimamizi bora wa rasilimali.

Hassan Salarieh Mkuu wa Shirika la Anga za Juu la Iran (ISA) amesisitiza kuwa satelaiti hizo zitatoa data muhimu kwa ufuatiliaji wa mazao, uchunguzi wa madini na ufuatiliaji wa dhoruba ya vumbi.