Kamanda wa IRGC: Usalama wa Ghuba ya Uajemi ni 'mstari mwekundu'
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i133910-kamanda_wa_irgc_usalama_wa_ghuba_ya_uajemi_ni_'mstari_mwekundu'
Naibu Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ametoa onyo kali kwa Marekani na washirika wake kuhusu Ghuba ya Uajemi na Mlango-Bahari wa Hormoz, akisema usalama wa njia hiyo ya maji ni "mstari mwekundu" wa Iran na misheni kuu ya IRGC.
(last modified 2025-12-04T10:49:36+00:00 )
Dec 04, 2025 07:47 UTC
  • Brigedia Jenerali Ali Fadavi
    Brigedia Jenerali Ali Fadavi

Naibu Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ametoa onyo kali kwa Marekani na washirika wake kuhusu Ghuba ya Uajemi na Mlango-Bahari wa Hormoz, akisema usalama wa njia hiyo ya maji ni "mstari mwekundu" wa Iran na misheni kuu ya IRGC.

Brigedia Jenerali Ali Fadavi ameeleza umuhimu wa kimkakati au wa kistratejia wa Mlango Bahari wa Hormoz na kusisitiza kuwa juu ya nafasi isioweza kujadiliwa ya eneo hilo kwa utulivu wa nishati duniani. 

Brigedia Jenerali Fadavi amesema kuwa mapipa ya mafuta zaidi ya milioni 20 kila siku yanapita katika njia hiyo ya maji na kwamba dunia inategemea nishati inayotoka katika Ghuba ya Uajemi. 

Naibu Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ametilia mkazo uhakika wa jiiografia na kisiasa kwamba  dunia nzima inatambua kuwa hakuna nchi nayoweza kupunguza mchango na nafasi ya Mlango Bahari wa Hormuz kwa kuzingatia hifadhi kubwa ya gesi ya Iran na Qatar. 

Brigedia Jenerali Ali Fadavi amesema jeshi la IRGC limejiandaa kikamilifu kulinda eneo hilo la kimakkati kwa nguvu zote kote baharini, ardhini na angani. "Ikiwa adui anataka kutishia usalama wetu, tutakabiliana nao kwa nguvu zetu zote."

Amelaani pia hatua za mabavu za Marekani na utawala wa Kizayuni na kuzitaja ndizo vyanzo vikuu vya 

vya ukosefu wa usalama wa kimataifa kuanzia Ghuba ya Uajemi hadi Amerika ya Kusini.