Rais Rouhani na Spika Larijani wapongeza jitihada za Wizara ya Intelijinsia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i13519-rais_rouhani_na_spika_larijani_wapongeza_jitihada_za_wizara_ya_intelijinsia
Rais wa Iran na Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran yaani bunge wamepongeza juhudi za pamoja za Wizara ya Intelijinsia katika kulinda amani na uthabiti na kukabiliana na vitisho.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Aug 18, 2016 14:07 UTC
  • Rais Rouhani na Spika Larijani wapongeza jitihada za Wizara ya Intelijinsia

Rais wa Iran na Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran yaani bunge wamepongeza juhudi za pamoja za Wizara ya Intelijinsia katika kulinda amani na uthabiti na kukabiliana na vitisho.

Akizungumza Jumatano hii na Waziri, Manaibu Waziri na Wakurugenzi wa Wizara ya Intelijinsia ya Iran, Rais Hassan Rouhani ameongeza kuwa lengo la serikali ya Iran ni kuwadhaminia wananchi amani na utulivu. Rais Rouhani ameashiria pia Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) na kubainisha kuwa maadui wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika uwanja wa nyuklia wanataka kuikwamisha nchi hii isimiliki elimu na tekonolojia ya nyuklia, na wakati huo huo kutoa mashinikizo kwa wananchi wa Iran kwa kisingizio cha miradi ya nyuklia.

Rais Rouhani amesema kuwa katika suala la JCPOA, Iran imedhihirisha na kuthibitisha kuwepo kwake katika uwanja wa elimu,  teknolojia, na katika soko la kimataifa la nishati ya nyuklia kutokana na miongozo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na uungaji mkono wa wananchi.

Kwa upande wake Ali Larijani Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu yaani Bunge amesema kuwa,  Wizara ya Intelijinsia ya nchi hii inafanya kazi nzuri katika  masuala ya kitelijinsia. Larijani ameashiria pia matukio ya Mashariki ya Kati na kuongeza kuwa uzushaji machafuko katika nchi za eneo kama huko Iraq, Syria Paksiatn, Uturuki na Misri ni kwa maslahi ya utawala wa Kizayuni. 

Ali Larijani Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge)