Reuters: Marekani ndiyo iliyoshambulia sherehe ya harusi nchini Iran
Baada ya kukiri New York Times, sasa ni zamu ya shirika la habari la Reuters kukiri na kuripoti kwamba, lina ushahidi wa wataalamu wanne wa silaha wanaothibitisha kuwa Marekani ndiyo iliyoshambulia moja kwa moja wananchi waliokuwa kwenye sherehe ya harusi huko Sirik kusini mwa Iran.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Mehr, licha ya Makamu wa Rais wa Marekani kujaribu kukataa kwamba wao ndio waliofanya jinai hiyo baada ya gazeti la Marekani la New York Times kutoa ripoti yenye ushahidi usiopingika kwamba ni Marekani ndiyo iliyoshambulia sherehe hiyo ya harusi, sasa shirika la habari Reuters pia limetoa ripoti ya kiuchunguzi kuhusu shambulio hilo la kikatili dhidi ya raia waliokuweko harusini katika mji wa Kohstek, Kaunti ya Sirik katika Mkoa wa Hormozgan wa kusini mwa Iran.
Ripoti ya Reuters inasema kwamba, mapitio ya picha na video zilizothibitishwa na wataalamu wanne wa silaha yanaonesha kwamba risasi zilizogonga ukumbi huo zilikuwa za Marekani. Uchunguzi huo wa Reuters pia umesema kuwa, ushahidi uliopatikana hauendani na madai kwamba kombora la Iran liligonga nyumba hiyo katika juhudi za kukabiliana na mashambulizi ya Marekani.
Jinai hiyo ya kutisha ya Marekani ilifanyika Jumanne jioni Septemba 1, 2026, wakati watu wwengi walipokuwa wamekusanyika katika nyumba moja huko Kohstek kusherehekea harusi.
Picha zilizopigwa baada ya shambulio hilo zinaonesha shimo kubwa kwenye paa la nyumba, uharibifu mkubwa wa uwanja wa nyuma na vipande vingi vya jengo.
Ripoti za awali zilionesha kuwa watu wanne waliuawa kikiwemo kitoto kidogo kimoja cha miaka minne na kwa uchache watu wengine 68 walijeruhiwa. Ripoti za baadaye zilionesha kuongezeka idadi ya waliouawa shahidi na kufikia watu watano.
Reuters iliwapatia video za tukio hilo wataalamu wanne wa silaha za kijeshi ili kuchunguza asili ya risasi hizo. Wataalamu watatu walisema risasi zilizotumika zilikuwa za Marekani, si kombora la Iran. Walisema umbo la shimo kwenye paa, muundo wa mripuko na aina ya uharibifu uliosababishwa na shambulio hilo unaonesha risasi hizo ziligonga jengo moja kwa moja. Mtaalamu wa nne amezungumzia uharibifu mkubwa uliofanyika na kuthibitisha kuwa hilo lilikuwa ni shambulio la moja kwa moja la jeshi la Marekani.