Dec 10, 2016 14:37 UTC
  • Wananchi wa Palestina ni wahanga wakuu wa jinai za Israel lakini mashirika ya haki za binadamu yananyamazia kimya jinai hizo.
    Wananchi wa Palestina ni wahanga wakuu wa jinai za Israel lakini mashirika ya haki za binadamu yananyamazia kimya jinai hizo.

Tume ya Haki za Binadamu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa mwito wa kuacha kutumiwa suala la haki za binadamu na asasi za kimataifa kama wenzo wa kuwadhibiti wengine kifikra, kiutamaduni, kisiasa na kiuchumi.

Tume ya Haki za Binadamu ya Iran imesema hayo katika taarifa yake kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu iliyoadhimishwa kote duniani hii leo na kusisitiza kwamba, utumiaji mbaya wa Uistikbari kwa udhaifu na mapungufu ya asasi za kimataifa sambamba na hatua ya madola ya kibeberu kuhodhi sekta ya vyombo vya habari, kivitendo imekwamisha juhudi za utetezi wa haki za binadamu.

Nembo ya Tume ya Haki za Binadamu Iran

Tume ya Haki za Binadamu ya Iran imesema pia katika taarifa yake hiyo kwamba, utawala haramu wa Israelo ukipata himaya na uungaji mkono wa Marekani na Ulaya umelizingira kila upande taifa la Palestina, umepora ardhi za Wapalestina na kuwapokonya wananchi hao madhulumu haki zao nyingi za kimsingi.

Sehemu nyingine ya taarifa ya Tume ya Haki za Binadamu ya Iran imeeleza kuwa, katika nchi za Syria na Iraq mamia ya maelfu ya watu wasio na hatia wanauliwa kwa umati na magaidi wanaoungwa mkono na Marekani, utawala haramu wa Israel na vile vile serikali za Ulaya na waungaji mkono wao katika eneo la Mashariki ya Kati kwa kushiriki moja kwa moja wanajeshi wa Marekani na wa barani Ulaya.

Kadhalika taarifa hiyo imeeleza kuwa, nchini Yemen karibu miaka miwili sasa wananchi wa nchi hiyo wanakabiliwa na wimbi la mashambulio kutoka kwa watu ambao ni waitifaki wakuu wa Marekani na Uingereza katika eneo la Mashariki ya Kati.

 

Tags