Meli za mafuta za Iran zarejea barani Ulaya
Meneja wa Shirika la Taifa la Meli za Mafuta la Iran amesema kuwa, meli za mafuta za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimerejea kwenye bandari za barani Ulaya.
Sirous Kianersi amesema hayo leo na kuongeza kuwa, hayo ni miongoni mwa mafanikio ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kuongeza kuwa, baada ya kuanza kutekelezwa makublianao hayo na kuondolewa vikwazo, safari za meli za mafuta za Iran kuelekea Ulaya zimeanza tena baada ya kuzuiwa wakati wa vikwazo.
Kianersi ameongeza kuwa, meli hizo za mafuta za Iran zimeanzia nchini Uhispania na tayari meli moja ya Shirika la Taifa la Meli za Mafuta la Iran imetia nanga kwenye bandari moja nchini Uhispania. Aidha amesema, safari za meli za mafuta za Iran zitatembelea pia nchi nyingine za Ulaya ikiwemo Uholanzi.
Tarehe 11 Januari 2016 Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki ilitoa ripoti kuhusu kutekeleza Iran ahadi zake kwa mujibu wa makubaliano ya nyuklia na upande wa pili yaani kundi la 5+1 ukaanza kuiondolea Iran vikwazo vinavyohusiana na nyuklia.