Kiwanda kikubwa zaidi cha kusaga nafaka Mashariki ya Kati chazinduliwa Iran
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezindua kiwanda kikubwa zaidi cha kusaga na kukoboa nafaka Mashariki ya Kati.
Kiwanda hicho kimezinduliwa leo asubuhi katika mkoa wa Alborz magharibi wa Tehran katika sherehe iliyohudhuriwa na Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Leo Jumanne ni siku ya kwanza ya maadhimisho ya 38 ya Alfajiri 10 za Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na hivyo uzinduzi huo umefanyika kwa munasaba huo.
Rais Rouhani ametembelea maeneo mbali mbali ya kiwanda hicho kinachojulikana kama Zar ambapo amefahamishwa kuhusu shughuli za kusaga na kukoboa nafaka hapo.
Hali kadhalika Rais Rouhani pia amezindua ujenzi wa kiwanda cha utengenezaji wa bidhaa za chakula kinachotokana na nafaka.
Mradi huo mkubwa utaondoa utegemezi wa kigeni katika kutengeneza aina mbali mbali za bidhaa za chakula kinachotokana na nafaka.