Zarif: Vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran havina natija iyokusudiwa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i26454-zarif_vikwazo_vya_marekani_dhidi_ya_iran_havina_natija_iyokusudiwa
Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran Mohammad Javad Zarif amesema vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran katika nyuga za kisaisa na kiuchumi vitaku na natija ambayo Wamarekani hawakukusudia.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Mar 16, 2017 03:55 UTC
  • Zarif: Vikwazo  vya Marekani dhidi ya Iran havina natija iyokusudiwa

Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran Mohammad Javad Zarif amesema vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran katika nyuga za kisaisa na kiuchumi vitaku na natija ambayo Wamarekani hawakukusudia.

Katika mahojiano yake na Televisheni ya Al Mayadeen, Zarif amesema vikwazo vya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran havina faida. Ameongeza kuwa, Iran inaamini kuwa, sababu iliyopelekea Marekani kushiriki katika mazungumzo ya nyuklia ya Iran na madola sita makubwa duniani ya kundi la 5+1 ni kuwa, serikali ya Barack Obama ilifanya tathmini kuhusu machaguao yote dhidi ya Iran na ikaona haina budi ila kuketi katika meza ya mazungumzo.

Zarif ameashiria namna Saudi Arabia na utawala wa Kizayuni wa Israel zilivyojaribu wazi wazi kuvuruga mazungumzo ya nyuklia ya Iran na kundi la 5+1 na kusema: "Baada ya kumalizika mazungumzo ya nyuklia mjini Geneva mwaka 2015, tawala hizo mbili kupitia Bunge la Kongresi la Marekani na njia zinginezo, zilijaribu kuzuia utekelezwaji wa mapatano hayo bila mafanikio."

Mawaziri wa kigeni wa nchi za 5+1, Iran na mkuu wa sera za kigeni EU baada ya mapatano ya nyuklia ya Iran

Zarif ameongeza kuwa, silaha za nyuklia za utawala wa Kizayuni wa Israel ni tishio kubwa zaidi kwa eneo la Mashariki ya Kati na dunia nzima na kubaini kuwa: "Utawala wa Israel ambao ni mkiukaji wa haki za Wapalestina na tishio kubwa zaidi la silaha za nyuklia duniani, hivi sasa unaendeleza uhasama dhidi ya mataifa ya eneo hilo hasa kwa kushambulia Lebanon, Palestina, Jordan, Syria na hata Misri."

Kwingineko katika mahojiano hayo, Zarif amesema Uturuki ni nchi muhimu na jirani ya Iran na kuongeza kuwa, "Uturuki ni nchi yenye taathira katika Mashariki ya Kati. Amesema, Ankara inapaswa kuchukua hatua kuhakikisha magaidi walioko Syria hawapati silaha kupitia ardhi yake.