Kiongozi Muadhamu: Ni dharura kuelewa nafasi ya mwanamke wa Kiislamu katika jamii
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i26594-kiongozi_muadhamu_ni_dharura_kuelewa_nafasi_ya_mwanamke_wa_kiislamu_katika_jamii
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, amesema kuna uwezekano mkubwa kwamba kumfanya mwanamke kuwa chombo cha anasa katika ulimwengu wa Magharibi, ni sehemu ya njama za Wazayuni kwa ajili ya kusambaratisha jamii ya mwanadamu.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Mar 19, 2017 13:02 UTC
  • Kiongozi Muadhamu: Ni dharura kuelewa nafasi ya mwanamke wa Kiislamu katika jamii

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, amesema kuna uwezekano mkubwa kwamba kumfanya mwanamke kuwa chombo cha anasa katika ulimwengu wa Magharibi, ni sehemu ya njama za Wazayuni kwa ajili ya kusambaratisha jamii ya mwanadamu.

Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi wa Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameyasema hayo leo kwa mnasaba wa sherehe ya siku ya kuzaliwa Bibi Fatima Zahraa (as) binti wa Mtume Muhammad (saw) alipokutana na wasomaji wa tungo za kumsifu Mtume na Ahlu Baiti wake (as).

Sambamba na kubainisha sababu ya kuenezwa nara za kama ile ya 'uadilifu na usawa wa kijinsia' katika nchi za Magharibi, amesema kuwa uadilifu ni kutambua vipawa na tunu alizopewa na Mwenyezi Mungu kuzistawisha.

Kiongozi Muadhamu alipokutana na wanawake wa Kiislamu kwa mnasaba wa leo

Kiongozi Muadhamu amesema kuwa, hii leo wasomi wa Magharibi na watu wanaonadi usawa wa kijinsia wanajutia hatua yao hiyo kutokana na makosa mengi yanayosababishwa na suala hilo. Vilevile ameashiria sira na harakati adhimu ya Bibi Fatima Zahraa (as), mwanamke mtukufu wa Kiislamu katika nafasi ya kiongozi halisi na wakati huo huo kama mke na mama wa aina yake na kumtaja kuwa ni kiigizo chema na kamili kwa ajili ya Waislamu.' 

Askari wanawake wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wakienzi nafasi chanya ya mwanamke wa Kiislamu

Ayatullah Ali Khamenei ameongeza kwa kusema kuwa, Bibi Fatima alikuwa dhihirisho la ukamilifu wa mwanamke wa Uislamu na alifikia daraja la juu la 'mwanamke wa Kiislamu' yaani kiasi cha kuitwa 'kiongozi'. Amesisitizia pia umuhimu wa kuelewa nafasi chanya ya mwanamke wa Kiislamu. 

Bibi Fatima Zahraa (as) Binti wa Mtukufu Mtume Muhammad (saw) alizaliwa siku kama ya leo miaka 1446 iliyopita yaani sawa na tarehe 20 Jamadu th-Thani mwaka wa nane kabla ya Hijiria.