Apr 15, 2017 07:31 UTC
  • Kongamano la Kimataifa la Haki za Binadamu lafunguliwa Tehran

Kongamano la Kimataifa la Kiislamu kuhusu Haki za Binadamu linafanyika hapa nchini Iran katika Chuo Kikuu cha Tehran.

Kongamano hilo la siku moja linatazamiwa kuwasilisha mafunzo na hoja za Kiislamu kuhusu haki za binadamu ili kuandaa ramani ya njia ya hoja hizo kuchukua nafasi ya sera na mtazamo wa Kimagharibi kuhusu haki hizo.

Wanazuoni, wanafikra na wasomi mbalimbali kutoka hapa nchini, Malaysia, Uingereza na Marekani wanatazamiwa kuwasilisha makala walizoandaa kuhusiana na kadhia hiyo.

Kongamano la Kimataifa la Kiislamu kuhusu Haki za Binadamu litajadili maudhui tatu kuu: Misingi ya Haki za Binadamu; Nukta za Kipekee za haki hizo; Na Vipaumbele.

Haki za Binadamu katika mizani ya Uislamu

Wasomi hao wa Kiislamu wanatazamiwa kuwasilisha hoja zinazoashiria umuhimu wa kufuatwa mafunzo ya Kiislamu  katika masuala ya Haki za Binadamu, na pia tofauti ya hoja hizo za Kiislamu na za Kimagharibi ambazo zinatawala sasa katika sehemu nyingi duniani.  

Hii ni katika hali ambayo, mapema mwezi uliopita, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Gutteres akihutubia kikao cha 34 cha baraza hilo mjini Geneva alikosoa vikali ukiukwaji wa haki za binadamu katika nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi na kutahadharisha kuhusu upuuzwaji wa haki hizo. Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi linaundwa na nchi za Saudi Arabia, Kuwait, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu, Oman na Bahrain. 

Tags