Qatar: Nchi za Ghuba zinahitajia kuwa na uhusiano mzuri na Iran
(last modified Thu, 18 May 2017 07:38:42 GMT )
May 18, 2017 07:38 UTC
  • Qatar: Nchi za Ghuba zinahitajia kuwa na uhusiano mzuri na Iran

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Qatar amesema kuwa, nchi za Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi zinahitajia kuwa na uhusiano mzuri na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Mohammed bin Abdulrahman Al Thani ameashiria hatua zilizopigwa na kuandaliwa mazingira ya kuweko mazungumzo ya pamoja baina ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi na kusema kuwa, baraza hilo linahitajia kuwa na uhusiano mzuri na Iran.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Qatar amesema hayo pambizoni mwa mkutano wa Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi uliofanyika mjini Riyadh Saudi Arabia na  na kusisitiza kwamba, nchi za kiarabu za eneo la Ghuba ya Uajemi zinahitajia kuwa na uhusiano mzuri na Tehran.

Bendera ya Iran

Mohammed bin Abdulrahman Al Thani amebainisha kwamba, Doha inaunga mkono mazungumzo yoyote ya pamoja kati ya Iran na Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi.

Kabla ya hapo pia, nchi za kuwait na Oman zilikuwa zimesisitiza juu ya umuhimu wa kufanyika mazungumzo ya pamoja ya kisiasa kati ya Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Daima Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikisisitiza juu ya kuweko mazungumzo yenye msingi wa kuheshimiana pande mbili na ujirani mwema katika eneo

Tags