Jun 08, 2017 06:53 UTC
  • Rouhani: Iran itajibu mapigo ya maadui kupitia umoja na mshikamano

Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu itasambaratisha njama za maadui kupitia umoja na mshikamano wa wananchi wa taifa hili.

Sanjari na kulaani mashambulio ya jana ya kigaidi hapa mjini Tehran, Rouhani amesema taifa la Iran litatumia umoja wa wananchi na nguvu zake kubwa za kiulinzi na kiusalama kuzima njama na mipango ya adui wa Jamhuri ya Kiislamu.

Dakta Rouhani amesema hujuma za jana hazitaikatisha tamaa nchi hii na kuifanya iachane na jitihada zake za kupambana na ugaidi na misimamo ya kufurutu ada katika eneo hili la Mashariki ya Kati.

Rais wa Iran amebainisha kuwa, maadui wa taifa hili walikerwa na mahudhurio makubwa ya wananchi wa nchi hii katika uchaguzi mkuu wa Mei 19, na ndiposa wakafanya juu chini kuwafadhili na kuwatuma hapa nchini wanachama wa magenge ya kigaidi na kitakfiri ili kuficha kusambaratika kwao katika eneo sambamba na kutaka kuporomoka thamani za Uislamu.

Maafisa usalama wakikabiliana na wanachama wa Daesh kwenye Bunge la Iran

Kadhalika Rais Hassan Rouhani amesisitiza kuwa ugaidi ni janga la kimataifa linalohitaji ushirikiano wa jamii ya kimataifa kupambana nalo.

Wakati huo huo, idadi ya watu waliouawa shahidi katika mashambulio mawili tofauti ya kigaidi ya jana hapa mjini Tehran yaliyolenga Bunge la Iran na Haram ya Imam Khomeini MA, imeongezeka na kufikia 16 wakiwemo wanawake watatu, kutoka 12 iliyoripotiwa awali,

Tags