Spika wa Bunge la Afrika Kusini awasili Iran
(last modified Fri, 01 Sep 2017 15:17:21 GMT )
Sep 01, 2017 15:17 UTC
  • Spika wa Bunge la Afrika Kusini awasili Iran

Spika wa Bunge la Afrika Kusini amewasili Tehran kwa ajili ya kufanya mazungumzo na maafisa wa ngazi za juu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Radio Tehran, Bi. Baleka Mbete amewasili hapa Tehran leo asubuhi akiongoza ujumbe wa ngazi za juu wa nchi yake. Alipowasilia mjini Tehran alilakiwa na Bi. Parvaneh Salahshuri, Mkuu wa Kamati ya Wanawake katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran. Kesho anatazamiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Ali Larijani, Spika wa Bunge la Iran na wawili hao watajadiliana uhusiano wa mabunge ya nchi hizi mbili pamoja na masuala mengine ya kieneo na kimataifa.

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Rais Hassan Rouhani wa Iran

Mwezi Aprili mwaka jana Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini aliitembelea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kufanya mazungumzo na viongozi wa ngazi za juu humu nchini. Uhusiano wa Pretoria na Tehran unatathminiwa kuwa mzuri na wa kidugu hasa kutokana na kuwa Iran iliunga mkono harakati za ukombozi wa Afrika Kusini wakati nchi hiyo ilipokuwa ikitawaliwa na utwala wa makabaru wabaguzi wa rangi. Nchi hizi mbili hivi sasa zina uhusiano mzuri na wa karibu wa kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.

Tags