Viongozi wa Iran na Pakistan wakutana Islamabad
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i3781-viongozi_wa_iran_na_pakistan_wakutana_islamabad
Rais Hassan Rouhani wa Iran na Nawaz Shariff Waziri Mkuu wa Pakistan wamekutana na kufanya mazungumzo na kujadili uimarishwaji uhusiano wa pande mbili hasa wa kiuchumi, masuala ya kieneo na kimataifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 25, 2016 11:21 UTC
  • Viongozi  wa Iran na Pakistan wakutana Islamabad

Rais Hassan Rouhani wa Iran na Nawaz Shariff Waziri Mkuu wa Pakistan wamekutana na kufanya mazungumzo na kujadili uimarishwaji uhusiano wa pande mbili hasa wa kiuchumi, masuala ya kieneo na kimataifa.

Mazungumzo hayo yamefanyika Ijumaa katika mji mkuu wa Pakistan, Islamabad punde baada ya Rais Rouhani kuwasili mjini humo.

Nchi hizo mbili zinatarajiwa kutia saini makubaliano katika sekta za biashara, uchumi, bima, utamaduni, elimu na afya.

Rais wa Iran anaitembelea Pakistan kwa mara ya kwanza tokea kufikiwa makubaliano ya nyuklia baina ya Iran na madola sita makubwa duniani hivi karibuni. Rouhani ambaye yuko Pakistan kwa ziara ya siku mbili anaongoza ujumbe wa ngazi za juu wa kisiasa na kiuchumi wa Iran unaojumuisha pia wafanyabiashara 60.

Akizungumza na waandishi habari mjini Tehran kabla ya kuelekea Islamabad, Rais Rouhani alisema uhusiano wa Iran na Pakistan ni muhimu kwani nchi mbili hizo zina mambo mengi yanayoziunganisha pamoja, ya kidini, kihistoria na kiutamaduni. Waziri Mkuu wa Pakistan aliitembelea Iran Januari 19 mwaka huu.