Boroujerdi: Afghanistan na Afrika walengwa wa baadaye wa Daesh
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i38885-boroujerdi_afghanistan_na_afrika_walengwa_wa_baadaye_wa_daesh
Mkuu wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Nje ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) ameeleza kuwa magaidi wa kundi la Daesh sasa wameelekea nchini Afghanistan na watajipenyeza pia katika nchi za Kafrika kama ilivyokuwa huko nyuma.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jan 12, 2018 14:27 UTC
  • Boroujerdi: Afghanistan na Afrika walengwa wa baadaye wa Daesh

Mkuu wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Nje ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) ameeleza kuwa magaidi wa kundi la Daesh sasa wameelekea nchini Afghanistan na watajipenyeza pia katika nchi za Kafrika kama ilivyokuwa huko nyuma.

Alauddin Boroujerdi amesema kuhusiana na mustakbali wa kundi la kigaidi la Daesh kwamba kundi hilo limepata pigo huko Syria na Iraq likiwa kama taasisi ya kijeshi na kisiasa; na kwamba Washington ilikuwa imeainisha muda wa kwa uchache miaka 20 ili kuweza kusambaratishwa kundi la Daesh. 

Mauaji ya umati yaliyofanywa na magaidi wa Daesh nchini Iraq

Mkuu wa Kamisheni ya usalama wa Taifa na Siasa za Nje ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amebainisha kuwa fikra za Kidaesh zitaendelea katika mkondo wake kwa miaka kadhaa na kwamba fikra hizo zimetokana na mafundisho ya Kiwahabi na uvumbuzi wa mashirika ya kijasusi ya Marekani na Uingereza.

Boroujerdi ameongeza kuwa, vitendo vinavyotekelezwa na  makundi ya kigaidi vitawagharimu waungaji mkono wa magaidi hao na kwamba kuwepo raia wa Ulaya katika kundi la Daesh kunadhihirisha ukweli huu kuwa nchi zilizousababishia matatizo ulimwengu wa Kiislamu hivi sasa zenyewe ndizo zinazotaabika na hujuma za kigaidi.