Araqchi: Marekani haiwezi kuchukua uamuzi peke yake kuhusu JCPOA
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i42920-araqchi_marekani_haiwezi_kuchukua_uamuzi_peke_yake_kuhusu_jcpoa
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amesema: makubaliano ya nyuklia ya JCPOA hayapo kwa ajili ya Marekani hata iamue kuchukua uamuzi wowote itakao kuhusu makubaliano hayo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 10, 2018 12:17 UTC
  • Araqchi: Marekani haiwezi kuchukua uamuzi peke yake kuhusu JCPOA

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amesema: makubaliano ya nyuklia ya JCPOA hayapo kwa ajili ya Marekani hata iamue kuchukua uamuzi wowote itakao kuhusu makubaliano hayo.

Sayyid Abbas Araqchi, amebainisha kuwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yanaihusu jamii ya kimataifa na nchi zote zilizoshiriki kwenye mazungumzo ya makubaliano hayo na kuongeza kwamba: JCPOA ni makubaliano muhimu, na Russia ni moja ya mihimili imara ya makubaliano hayo.

Akizungumza katika mahojiano na kanali ya televisheni ya Russia Today, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amefafanua kwamba: Russia ilikuwa moja ya pande kuu katika mazungumzo ya nyuklia na Iran; na kama makubaliano ya JCPOA yanavyoihusu Iran ndivyo yanavyoihusu pia Russia na nchi nyingine wanachama wa kundi la 5+1.

Wanadiplomasia waandamizi wa Iran na nchi zinazounda kundi la 5+1 baada ya kufikia makubaliano ya JCPOA

Makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA yaliyofikiwa kati ya Iran na kundi la 5+1 linalojumuisha Uingereza, Ufaransa, Russia, China, Marekani na Ujerumani yalianza kutekelezwa Januari 2016, hata hivyo Marekani imekuwa kila mara ikikwepa kutekeleza wajibu wake kuhusiana na makubaliano hayo.

Araqchi aidha ameashiria matukio yanayojiri nchini Syria na kueleza kwamba: utawala wa Kizayuni wa Israel unataka kuzidisha hali ya wasiwasi katika eneo la Mashariki ya Kati, kwa hivyo pande zote husika katika mgogoro wa Syria zinapaswa kuwa macho sana na kadhia hiyo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran vilevile amesema uhusiano wa Iran na Russia una umuhimu mkubwa na akabainisha kuwa uhusiano huo unajumuisha nyanja mbalimbali zikiwemo za kisiasa, kiuchumi na kistratejia.../