Muhammad Javad Zarif: Serikali ya Marekanin imefilisika kimaadili
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i43074-muhammad_javad_zarif_serikali_ya_marekanin_imefilisika_kimaadili
Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa njama za Marekani za kutaka kurejesha vikwazo dhidi ya Iran na kusema kuwa, serikali ya Washington imefilisika kimaadili.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 13, 2018 23:47 UTC
  • Muhammad Javad Zarif: Serikali ya Marekanin imefilisika kimaadili

Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa njama za Marekani za kutaka kurejesha vikwazo dhidi ya Iran na kusema kuwa, serikali ya Washington imefilisika kimaadili.

Dakta Muhammad Javad Zarif ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter ambapo sambamba na kuashiria matamshi ya Mike Pompeo aliyependekezwa kushika wadhifa wa Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Marekani aliyoyatoa katika kikao cha Kamati ya Mahusiano ya Kigeni ya Baraza la Seneti iliyokuwa ikijadili ustahiki amesema kuwa, kufilisika kkimaadili kwa Marekani kumedhihirika wazi katika matamshi ya Mike Pompeo.

Pompeo alisema katika kikao hicho kwamba: Kabla ya makubaliano ya nyuklia Iran haikuwa ikielekea upande wa kutengeneza silaha za nyuklia na hivi sasa pia kwa ninavyojua mimi hakuna ishara zozote zinazoonyesha kwamba, kama makubaliano ya nyuklia ya JCPOA hayatakuweko basi Iran itaelekea upande wa kutengeneza silaha za nyuklia.

Mike Pompeo aliyendekezwa kushika nafasi ya Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Marekani

Makubaliano ya nyuklia kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kundi la 5+1 linaloundwa na nchi za Russia, Ufaransa, Uingereza, China, Marekani pamoja na Ujerumani yalianza kutekelezwa Januari mwaka 2016.

Licha ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kufungamana kikkamilifu na makubaliano hayo tangu yapasishwe Julai 2015 na hata ripoti zote za Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) kuthibitisha kwamba, Iran imefungamana kikamilifu na makubaliano hayo, lakini Marekani imekuwa ikiamiliana na Tehran kwa vitisho na vikwazo na kukwepa kutekeleza majukumu yake.