Jeshi la Iran lazima shambulio la kigaidi katika mpaka na Pakistan
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i43258-jeshi_la_iran_lazima_shambulio_la_kigaidi_katika_mpaka_na_pakistan
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran SEPAH limefanikiwa kuzima jaribio la shambulizi la kigaidi karibu na mpaka wa nchi hii na Pakistan, ambapo magaidi watatu wameangamizwa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 17, 2018 09:43 UTC
  • Jeshi la Iran lazima shambulio la kigaidi katika mpaka na Pakistan

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran SEPAH limefanikiwa kuzima jaribio la shambulizi la kigaidi karibu na mpaka wa nchi hii na Pakistan, ambapo magaidi watatu wameangamizwa.

Katika taarifa, SEPAH imesema kundi la kigaidi kutoka Pakistan mapema leo lilishambulia mnara wa usalama wa Gadi ya Mpaka ya Iran katika mji wa Mirjaveh, kusini mashariki mwa mkoa wa Sistan na Baluchestan, lakini limekabiliwa vikali.

Kadhalika wanajeshi wawili wa SEPAH na askari mmoja wa Gadi ya Mpakani wameuawa shahidi katika makabiliano hayo, huku wengine wawili wakijeruhiwa, baada ya gari lao kukanyaga bomu la kutegwa ardhini.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran liko makini mno katika kulinda usalama wa mipaka yake huku likistafidi na uzoefu wake wa zaidi ya miongo 3 katika uwanja huo, na kwamba njama hizo za magaidi zitaendelea kugonga mwamba.

Mpaka wa Iran na Pakistan

Mapema mwaka huu, Waziri wa Usalama wa Iran, Mahmoud Alavi alitangaza kuwa vyombo vya usalama hapa nchini vimewakamata magaidi kadhaa waliokuwa wamepanga kutekeleza mashambulizi katika maeneo 50 nchini Iran.

Wanachama wa kundi hilo la kigaidi walikiri kwamba walifadhiliwa na Saudi Arabia na Marekani.