Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani yaanza mjini Tehran
Mashindano ya Kimataifa ya 35 ya Qur'ani Tukufu yameanza leo mjini Tehran yakiwashirikisha wawakilishi wa nchi 84 kutoka maeneo yote ya dunia.
Mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani yanayofanyika kwa kaulimbiu ya "Kitabu Kimoja, Umma Mmoja" sambamba na kuanza sherehe za mwezi huu mtukufu wa Shaabani yanawachuanisha maqari na wasomaji 258 kutoka nchi 84 na yataendelea hadi tarehe 26 mwezi huu wa Aprili.
Mashindano ya sasa ya kimataifa ya Qur'ani yanafanyika katika vitengo vitano vya wanaume, wanawake, vipofu, wanafunzi wa vyuo vikuu na wanafunzi wa vyuo vya kidini.

Katika upande wa wanawake mashindano hayo yanawashirikisha maqari kutoka nchi 28.
Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran ambayo ni tukio kubwa zaidi linalohusiana na Qur'ani katika Ulimwengu wa Kiislamu yatafanyika kwa kipindi cha siku 7.