Wanachuo na wahadhiri nchini Iran walaani matamshi machafu ya rais wa Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i44274-wanachuo_na_wahadhiri_nchini_iran_walaani_matamshi_machafu_ya_rais_wa_marekani
Wahadhiri, wanachuo na jumuiya za wanachuo nchini wameandamana na kukusanyika mbele ya 'Pango la Ujasusi' la uliokuwa ubalozi wa Marekani hapa mjini Tehran kulaani maneno machafu aliyotoa rais wa Marekani.
(last modified 2026-03-03T12:46:59+00:00 )
May 09, 2018 22:53 UTC
  • Wanachuo na wahadhiri nchini Iran walaani matamshi machafu ya rais wa Marekani

Wahadhiri, wanachuo na jumuiya za wanachuo nchini wameandamana na kukusanyika mbele ya 'Pango la Ujasusi' la uliokuwa ubalozi wa Marekani hapa mjini Tehran kulaani maneno machafu aliyotoa rais wa Marekani.

Wahadhiri na wanachuo hao walikusanyika jana mbele ya uliokuwa ubalozi wa zamani wa Marekani na kutoa sha'ar za "Mauti kwa Marekani".

Wanaakademia wa vyuo vikuu vya mjini Tehran aidha wametangaza kuiunga mkono kwa kila hali hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyotoa hapo jana.

Wanachuo wa Chuo Kikuu cha Allamah 'Taba'tabai na wa Chuo Kikuu cha Ufundi cha Amir Kabir nao pia walikusanyika katika maeneo ya vyuo vyao baada ya Sala za Adhuhuri na Alasiri hapo jana na kulaani hotuba yenye lugha chafu aliyotoa Rais Donald Trump wa Marekani na uamuzi wa nchi hiyo wa kujitoa kwenye makubaliano ya kimataifa ya JCPOA.

Rais Donald Trump wa Marekani

Katika mji wa Mashhad ulioko kaskazini mashariki mwa Iran, wanachuo, vijana na jamaa wa familia za mashahidi, nao pia walikusanyika kulalamikia uamuzi wa Marekani wa kujitoa katika makubaliano ya JCPOA na kusisitiza kutekelezwa miongozo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyotoa kupitia hotuba yake ya hapo jana.

Shura ya Uratibu ya Jumuiya ya Tablighi ya Kiislamu ya Iran imetoa taarifa ya wito kwa wananchi wote kushiriki kwenye maandamano ya umma dhidi ya Marekani yatakayofanyika nchini kote hapo kesho baada ya ibada ya kimaanawi na kisiasa ya Sala ya Ijumaa.

Kwa kutoa madai kwamba makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCOPA) hayajawa na tija, sambamba na kuzusha madai yasiyo na msingi dhidi ya Iran, siku ya Jumanne usiku, rais wa Marekani Donald Trump alisaini amri ya kuiondoa nchi yake katika makubaliano hayo. Marekani imechukua hatua yake hiyo ya upande mmoja huku nchi nyingine tano zilizosaini makubaliano ya nyuklia na Iran pamoja na nchi nyingine nyingi duniani zikitangaza uungaji mkono wao kwa makubaliano hayo ya kimataifa.../