Marekani imekiuka sheria kwa kujiondoa katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i44322-marekani_imekiuka_sheria_kwa_kujiondoa_katika_mapatano_ya_nyuklia_ya_jcpoa
Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa taarifa rasmi kufuatia kufuatia hatua ya Marekani kukiuka sheria na kujiondoa katika mapatano ya nyuklia yajulikanayo kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji JCPOA.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
May 11, 2018 00:15 UTC
  • Marekani imekiuka sheria kwa kujiondoa katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA

Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa taarifa rasmi kufuatia kufuatia hatua ya Marekani kukiuka sheria na kujiondoa katika mapatano ya nyuklia yajulikanayo kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji JCPOA.

Taarifa hiyo imesema: "Kitendo cha Rais wa Marekani kujiondoa kinyume cha sheria katika mapatano ya JCPOA ni hatua ya mwisho katika vitendo kadhaa vya ukiukwaji wa JCPOA ambao umekuwa ukitendwa na Marekani." Taarifa hiyo imesema matamshi kishenzi ya Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya taifa adhimu la Iran ni ishara ya kilele cha ujinga na ujahilia sambamba na ukosefu wa busara na tuhuma zisizo na msingi dhidi ya serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Taarifa hiyo imesema hatua hiyo ya Trump inaufaidisha tu utawala wa Kizayuni wa Israel ambao kwa sera zake vamizi umeenza ghasia katika eneo. Aidha taarifa hiyo imesema Marekani na mutifaki wake Mzayuni ni wakiukaji wakubwa wa haki za binadamu katika hali ambayo anatoa tuhuma za kichekesho dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Taarifa hiyo imeashiria namna ambayo Marekani imekuwa ikivunja na kujiondoa katika miktaba ya kimataifa kama vile mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi wa Paris na mkataba wa kibiashara wa Bahari ya Pasifiki na kusema:  "Kujiondoa katika JCPOA kutapelekea Marekani iendelee kujipotezea itibari katika uga wa kimataifa.

Rais Hassan Rouhani akilihutibia taifa baada ya Marekani kuniondoa JCPOA

 

"Kinyume cha ilivyo Marekani, Iran imekuwa ikitekeleza ahadi zake za kimataifa na hata Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki, IAEA, katika ripoti zake 11 umethibitisha hilo," imesema taarifa hiyo. Aidha Iran imesema ina haki ya kuchukua hatua mkabala kwa maslahi yake  baada ya Marekani kujiondoa katika JCPOA . Halikadhalika taarifa hiyo imesema nchi tano zilizosalia katika JCPOA ambazo ni China, Russia, Ufaransa, Uingereza na Ujerumani, hasa nchi hizo tatu za Ulaya, zinapaswa kuchukua hatua za lazima kulinda mapatnao hayo na kuyatekeelza bila masharti.

Taarifa hiyo ya serikali ya Iran pia imeashiria hatua ya Marekani kuziuzia nchi za Kiarabu silaha zenye kugharimu mabilioni na dola na kwa njia hiyo kuligeuza eneo la Asia Magharib kuwa sawa na ghala la baruti na kusema: "Marekani inaingilia mambo ya ndani ya eneo na kufuatilia sera ghalati zenye kuchochea hali ya mambo, kuibua makundi ya kigaidi na kusababisha vita, uharibufu na mauaji ya watoto." Kwa msingi huo Marekani haiwezi kudai eti Iran inavuruga eneo katika hali ambayo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa na nafasi kubwa katika kuzisaidia nchi za Syria na Iraq kuangamiza magaidi waliolelewa na Marekani yenywe.